Pages

Basi la Machame lapinduka eneo la Msata mkoa wa pwani

 Watu wawili wamejeruhiwa na wengine kadhaa kunuaurika baada ya basi walilokuwa wakisafiria kupinduka katika eneo la Msata, mkoani Pwani.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema kuwa waliojeruhiwa ni pamoja na dereva wa basi hilo, mali ya kampuni ya Machame, lenye namba za usajili T 712 DCL.
Basi hilo lililokuwa linatoka Dar kuelekea Arusha, lilipinduka kufuatia kupasuka kwa tairi ya mbele upande wa kulia, ambapo liliacha njia na kugonga kingo za barabara.

Mwingine ni mwanamke ambaye jina lake pia halijaweza kupatikana, ambaye alikuwa abiria katika basi hilo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)