Pages

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII AFRIKA MASHARIKI NA KATI (ECASSA)

 Katibu Mkuu wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, (TSSA), Meshack Bandawe, (katikati), akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa idara ya Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, Februari 14, 2016. Pamoja na mambo mengine Bandawqe alisema, mkutano wa mwaka wa Muungano wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Mamlaka za Usimamizi Sekta za Hifadhi za Jamii kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (ECASSA), utafanyika nchini kuanzia Februari 18mwaka huu 2016. (Kushoto) ni Naibu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Vincent Tiganya, na kulia ni mjumbe wa kamati ya waandaaji wa mkutano, Rehema Kabongo.
NA
K-VIS MEDIA/Khalfan Said
TANZANIA itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Muungano wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (Pensheni na afya), na Mamlaka za usimamizi wa sekta za hifadhi ya Jamii za nchi za Afrika Mashariki na Kati, Katibu Mkuu wa Chama Cha Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Tanzania, (TSSA), Meshack Bandawe Amesema.
Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Februari 14, 2016 kwenye ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO jijini Dar es Salaam, Bandawe alisema, mkutano huo utakuwa wa siku mbili na utaanza Februari 18 na kukamilika Februari 19 mwaka huu 2016. “Mkutano utafanyika ukumbi wa mikutano wa Benki Kuu (BoT) na utafunguliwa na Mh. Makamu
wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.” Alisema Bandawe

Alisema, madhumuni ya mkutano huo ambao hufanyika kila mwaka kwa mzunguko wan chi wanachama, ni kujadili sera zinazohusiana na sekta ya hifadhi ya jamii. “Washiriki hupokea mada zinazowasilishwa na wataalamu mbalimbali, kuzichambua na kuzijadili kabla ya kuweka maazimio kwa ajili ya kuboresha sekta ya hifadhi ya jamii katika nchi wanachama.
Kwa mara ya kwanza mkutano kama huu ulifanyika jijini Mwanza na kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu ni “Kuwiania sera za Kiuchumi, upatikanaji wa ajira na maendeleo ya sekta ya hifadhi ya jamii katika Afrika Mashariki na Kati”.
 Waandishi wakiwa kazini

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)