Pages

TAMASHA LA ‘AMSHA MAMA TANZANIA’ KUFANYIKA MACHI 5 KATIKA UWANJA WA MWEMBEYANGA TEMEKE JIJINI DAR

WATANZANIA  wametakiwa kujitokeza kwa wingi katika Tamasha la ‘Amsha Mama Tanzania’ linalotarajiwa kufanyika Machi 5 katika uwanja wa Mwembeyanga Temeke  jijini  Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mkurugenzi wa Kampuni ya  Candy record yenye makao Mkuu yake nchini Kenya ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo Joe Kariuki amesema wameamua kuleta tamasha nchini ili kuwapa fursa akina mama wa Tanzania kujiinua kiuchumi .
“ Akina mama mjitokeze kwa wingi katika tamasha hili mahususi kwenu kwa kuwa  mtapata fursa mbalimbali na mtaweza kupata mambo mbalimbali ikiwemo elimu” .Alisema Kariuki.

Kwa upande wake balozi wa Amsha Mama nchini Khalid Ramadhani (Tundaman), amewaomba wakinamama wachangamkie fursa kwani watajifunza mambo mengi
“Nawaomba Mama zangu mjitokeze kwa wingi kwani tumepata bahati ya pekee ya kupendelewa kuletewa tamasha nchini kwani ni adimu kutokea,” .alisema Tundaman.

Tamasha hilo linatarajiwa kufanyika pia katika uwanja wa Ranchi ya Kedong uliopo jiji la Naivasha nchini Kenya marchi 25-27 huku likitarajia kukutanisha akinamama kutoka nchi zote za Afrika .

Aidha kutakuwa na burudani kutoka kwa wasanii kama vile Juma Kassim  ‘’Juma Nature’’, Khadija Kopa, Roma Mkatoliki, Young Killer, Msagasumu, Man fungo,Sharo mwamba,Q-Chief,Mr Blue,Snura,Tundaman,na Ally Choki.
Tamasha la Amsha Mama linatarajiwa kukutanisha akinamama mbalimbali kwa lengo la kujifunza kuhusu kujikwamua kiuchumi kwani wao ndio chachu ya mafanikio.
Alisema wamejipanga kuwapa  radha tofauti  watoto wa temeke na majirani zake ,hasa kwa akina mama kupata fursa ya kujielewa na kujitambua hasa katika kuendeleza familia zao.
Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)