Pages

Soma kisa hiki cha Paka kina funzo ndani yake



Mama mmoja alimuamini sana paka wake kiasi Cha Kuwa anamwachia Mtoto wake mchanga ili ambembeleze wakati yeye akienda shamba. Siku zote aliporudi alimkuta paka yuko Jirani Na mwanaye akimbembeleza akiwa Salama salmini.

Lakini siku moja aliporudi kutoka kwenye shughuli zake Kama ilivyo kawaida yake; Alikuta kitanda kimevurugwa; nguo aliyokuwa amemvisha mtoto ilikuwa imechanwachanwa vipande Na ina Damu alipochungulia uvunguni ndipo akamuona paka Na paka naye alipomuona huyo mama akajitokeza Huku akiwa anachuruzika Damu midomoni mwake. Mama akajua kwamba paka kamla au kamuua mwanaye kwa hiyo akachukua gongo la mti akampiga nalo pigo moja tu paka akafa.

Huku akitweta alipoangalia pembeni mwa kitanda akiwa ameviringishwa ndani ya shuka; alimuona mwanaye akiwa mzima kabisa. Alipoangalia kwa kina chini ya kitanda akaona kichwa Cha joka kikiwa kimetenganishwa Na kiwiliwili chake Na baadhi ya vipande Vya mwili wa Nyoka akaviona ndipo akagundua Kuwa kumbe paka wake alikuwa Na vita Kali ya kumtetea Mtoto wake. Akajuta kwa sababu asingeweza kumpa uhai paka wake aliyemsaidia kunusuru uhai wa mwanaye. Akatoa kilio kikubwa Huku akimshika mkononi paka wake aliyepigana kufa Na kupona kuokoa uhai wa Mtoto wake. Majuto Mjukuu. Alikuwa tayari keshafanya kosa la kumuua paka wake mwaminifu sana, kabla ya kujipa muda zaidi wa kutafakari.

Ndugu Yangu Nakusihi Ni muhimu sana kujipa muda wa kutafakari kwa kina kuhusu Jambo lolote linalotuijia mbele yetu Na hatimaye tusiumize nyoyo zetu baadaye kwa kujilaumu kama Yule mama alivyolia kwa kumuua haraka haraka paka wake ambaye alikuwa mwaminifu sana. Asanteni sana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)