Pages

Naibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla atembelea kambi ya wagonjwa wa kipindupindu ya Mt. Lucas Mkoani Iringa

Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla mapema leo Februari 15, ametembelea kambi ya Wagonjwa wa Kipindupindu pamoja na wale waliokumbwa na mafuriko katika kijiji Mboliboli Kata Pawaga Wilayani Iringa ambapo hadi sasa kambi hiyo ina wagonjwa 40 huku zaidi ya wagonjwa 223 walilipotiwa kuugua tangu kipindupindu kimeanza katika eneo hilo.

Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza wakati wa kutoa taarifa yake kwa Naibu Waziri Dk. Kigwangalla aliyetembea ya Mkuu wa mkoa huyo, alimweleza kuwa kati ya wagonjwa hao 223, wagonjwa 17 ni watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, Mbali na hao hadi sasa yamesababisha kifo kimoja.

Ugonjwa huo umeelezwa kuwa umewakumba kutokana na mvua zilizonyesha na kubomoa vyoo na kutapanya kinyesi hali iliyopelekea ugonjwa huo kusambaa Zaidi katika makazi ya wananchi hao.

Hadi sasa eneo hilo limekumbwa na maji huku wananchi wakilazimika kuyakimbia makazi yao na hata kuzungukwa na maji karibu eneo kubwa na usafiri wa watoa huduma kuwa wa shida ikiwemo kutumia boti maalum ama chopa.
Mkoa huo ulikumbwa na mvua mnamo Februari 3 hadi leo bado maji yameendelea kuzingira maeneo ya vijiji hivyo.
RC IringaMkuu wa mkoa wa Iringa Bi.Amina Masenza akitoa taarifa kwa Naibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa kwanza waliokaa kushoto) wakati alipotembelea ofisini hapo. Wengine ni watendaji wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (waliokaa kulia).
DSC_0468Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitoa taarifa namna ya kamati yake ilivyopambana usiku na mchana na hatua waliofikia katika kuakikisha kipindupindu kinakwisha katika eneo hilo huku wakiendelea na jitihada za kupambana na mafuriko ikiwemo kuokoa wananchi waliobakia eneo hilo.
kigwangaNaibu Waziri wa Afya, Dk. Kigwangalla, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa mara baada ya kumaliza kwa mazungumzo na taarifa fupi juu ya ugonjwa wa kipindupindu kwenye maeneo ya vijiji vya Mkoa huo ambapo hadi leo wamefikia jumla ya wagonjwa 40.
dk kigwanomicNaibu Waziri wa Afya, Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela wakiwasili katika uwanja wa Ndege wa Nduli, Iringa tayari kwa kuelekea kupanda Chopa kuelekea kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
dk kigwangazWakielekea katika Chopa maalum ya jeshi la Polisi kwa ajili ya kuwafikia wananchi waliozingirwa na maji ya mafuriko pamoja na ugonjwa wa kipindupindu.
Dk kigwaziiNaibu Waziri wa Afya, Dk.Kigwangalla akipanda Chopa tayari kuelekea kwenye eneo lililokumbwa na mafuriko katika vijiji vya Mbolimboli, Pawaga, Mkoani Iringa. (Picha zote na Andrew Chale,modewjiblog-Iringa).

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)