Pages

Man Utd kuvaana na Liverpool kwenye ligi ya Europa

Man Utd
Image copyrightGetty
Image captionMan Utd hawajawahi kukutana na Liverpool ligi ya Ulaya
Manchester United watakutana na mahasimu wao wa jadi Liverpool katika hatua ya 16 bora katika Europa League.
Tottenham wamepewa miamba wa Bundesliga Borussia Dortmund baada ya droo kufanywa.
Valencia, walio chini ya Gary Neville, watakutana na wapinzani wao katika La Liga Athletic Bilbao.
SevillaImage copyrightAP
Image captionSevilla wameshinda Europa League miaka miwili mtawalia
Sevilla, walioshinda kombe hilo miaka miwili iliyopita, wataanza ugenini dhidi ya Basel katika uwanja wa St Jakob-Park, ambao pia utaandaa fainali.
Mechi hizo zitachezwa Alhamisi tarehe 10 na 17 Machi.
Washindi wa ligi hiyo watafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mwaka ujao.
United, ambao hawajawahi kushinda Europa League, walilaza FC Midtjylland kwa jumla ya mabao 6-3.
RashfordImage copyrightGETTY
Image captionRashford alifungia Manchester United mabao mawili
Marcus Rashford alifunga mabao mawili mechi yake ya kwanza kabisa kuwachezea mechi ya marudiano ambayo United walishinda 5-1 usiku wa Alhamisi.
Liverpool chini ya Jurgen Klopp walisonga kwa kulaza Augsburg 1-0 kwa jumla, bao la pekee likifungwa na James Milner Alhamisi.
Klabu hiyo ilishinda kombe la zamani lililokuwa likijulikana kama Kombe la Uefa mara tatu 1973, 1976 na 2001.
Itakuwa mara ya kwanza kwa United na Liverpool kukutana ligi ya Ulaya.
Droo kamili ya Europa League hatua ya 16
  • Shakhtar Donetsk v Anderlecht
  • Basel v Sevilla
  • Villarreal v Bayer Leverkusen
  • Athletic Bilbao v Valencia
  • Liverpool v Manchester United
  • Sparta Prague v Lazio
  • Borussia Dortmund v Tottenham
  • Fenerbahce v Braga
FernabahceImage copyrightAFP
Image captionFernabahce watakutana na Braga. CHANZO BBC SWAHILI

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)