Mratibu wa mpambano wa masumbwi Rajabu Mhamila 'Super D' katikati akiwa na mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka utakaofanyika uwanja wa ndani wa Taifa Picha na SUPER D BOXING NEWS |
Bondia Mada Maugo kushoto akipokea sehemu ya malipo ya awali kutoka kwa mratibu Rajabu Mhamila 'Super D' wa mpambano wake na Abdallaha Pazi. utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka Picha na SUPER D BOXING NEWS
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Mada Maugo na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa taifa mpambano wa raundi nane KG 76.
akizungumza wakati wa kutiliana saini mikataba hiyo kocha wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ambaye ni mratibu wa mpambano huo amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo ambao wanatamba katika tasnia ya masumbwi nchiniili wapenzi wa mchezo wa masubwi waburudike siku hiyo ya sikukuu ya pasaka
Mbali na mpambano uho siku hiyo bondia chipkizi anaekuja kwa kasi zaidi katika mchezo wa masumbwi Vicent Mbilinyi anaetokea katika Super D Boxing Promotion atakae pambana na Mwinyi Mzengela mpambano wa KG 63 raundi nane mpambano mwingine utawakutanisha bondia Cosmas Cheka na Mohamed Matumla na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba
siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)