Pages

WANANCHI WASHIRIKI UKARABATI WA BARABARA YA MUTURU KATIKA HALMASHAURI YA MJI WA TARIME.

Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Chira Kata ya Kenyamanyoro katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu (Remaghinga) iliyopo Mtaa wa Buguti Kata ya Rebu ambayo inayotegemewa na Wakazi Kata zote mbili za Kenyamanyori na Rebu hatika halmashauri hiyo.

Zoezi hilo limefanyika leo Januari 02,2016 ambapo wananchi hao walikuwa wakifanya ukarabati wa kujaza moramu katika maeneo yaliyochimbika kutokana na maji ya mvua pamoja na kuchimba mitaro kwa ajili ya kupitisha maji wakati wa mvua.

"Hii barabara ni kama imesahaulika na Halmashauri ingawaje ni mhimu sana kwani tegemeo kwa wananchi pamoja na shughuli mbalimbali kama vile ujenzi kwa kuwa hapo ng'ambo kuna shughuli za uchimbaji wa mawe hivyo malori huwa yanapita hapa kwa ajili ya kwenda kufuata mawe hayo kwa ajili ya ujenzi katika maeneo mbalimbali ya mji". Alibainisha mmoja wa wananchi hao na kuongeza kuwa imekuwa kawaida yao kufanya ukarabati wa aina hiyo pindi barabara hiyo inapoharibika.

Hatua ya Wananchi hao inapaswa kuigwa na wanajamii wengine pamoja na viongozi wenye dhamana ya kuwasimamia katika masuala ya maendeleo wakiwemo watendaji na wenyeviti wa serikali za mitaa kwani maendeleo yanapatikana haraka zaidi ikiwa wanajamii watashiriki ipasavyo katika shughuli zao za kimaendeleo badala ya kuishia kulalamika mitaani.
Na:George Binagi-GB Pazzo @Binagi Media Group
Baadhi ya Wananchi wa Mtaa wa Chira katika Halmashauri ya Mji wa Tarime Mkoani Mara wakishiriki zoezi la ukarabati mdogo wa barabara ya Muturu (Remaghinga) inayotegemewa na Wakati Kata za Kenyamanyori na Rebu hatika halmashauri hiyo.
Hii ndiyo dhana halisi ya Maendeleo
Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
Wanajamii wajiwekee utaratibu wa kutatua kero mbalimbali za kimaendelo katika maeneo/mitaa yao
Maendeleo yanaanza na kila mmoja katika jamii
Kulalamika mitaani si suluhisho la utatuzi wa kero mbalimbali katika jamii
George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
George Binagi-GB Pazzo ambae ni Mwanahabari na Mmiliki wa Mtandao wa Binagi Media Group (Mwenye jembe) nae alishiriki zoezi hilo
Barabara ya Muturu (Remaghinga) ni tegemeo kwa wananchi wa kila rika wakiwemo watoto 
Hakika barabara hii imeharibika sana na inahitaji ushirikiano zaidi ili kuweza kurejea katika hali nzuri
Picha hii inaonesha baadhi ya makazi ya watu wanaotegemea barabara hiyo ya Muturu (Remaghinga) ambapo imepigwa kutoka ng'ambo ya pili inakoelekea barabara hiyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)