Pages

Wafanyakazi wa TBL Mbeya wapatiwa elimu ya jinsia

 Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba akitoa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL Mbeya .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini
 Afande Prisca akiwazungukia washiriki wakati wa semina
 Baadhi wa wafanyakazi wa TBL Mbeya wakimsikiliza afande Prisca wakati huo huo wakipata chakula cha mchana.
5.Baadhi wa wafanyakazi wakiburudika na kupata maarifa baada ya saa za kazi wakati wa mafunzo hayo awamu ya jioni
Baadhi wa wafanyakazi wakiburudika na kupata maarifa baada ya saa za kazi wakati wa mafunzo hayo awamu ya jioni
Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group katika kiwanda cha Mbeya leo wamepatiwa  semina kuhusiana na masuala ya jinsia na Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni Inspekta Prisca Komba.
 
Katika semina hiyo wafanyakazi waliweza kujua masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya kijinsia ambapo pia walipata fursa ya kuuliza sheria na masuala ya jinsia kutoka kwa mkufunzi huyo kutoka Jeshi la Polisi.
 
Baadhi ya wafanyakazi walioshiriki mafunzo hayo walisema kuwa yameweza kuwafumbua macho kujua masuala mbalimbali yatakayowasaidia katika maisha yao ya kila siku wanapokuwa sehemu za kazi na katika maisha ya kawaida na familia zao wanapokuwa wameishatoka kazini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)