Pages

UNESCO YAFANYA KONGAMANO LA KUJADILI MPANGO WA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU (ESDP) KWA MWAKA 2017 - 2021

IMG_1467
Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu, Prof. Eustella Bhalalusesa akizungumza na waandishi wa habari katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP). Kushoto ni Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues. (Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
IMG_1499
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na kongamano hilo la siku mbili linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa NACTE jijini Dar es Salaam.
Na Rabi Hume wa Modewjiblog
Katika kuhakikisha elimu ya Tanzania inakua yenye ubora zaidi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limepanga kuisaidia Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi kuandaa Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP), mpango ambao umelenga kusaidia serikali ya Tanzania kutengeneza maudhui na mikakati ya kuendeleza elimu kwa upande wa Tanzania bara.
Akizungumzia mpango huo katika kongamano la siku mbili la kutambua vipaumbele vinavyotakiwa katika kuandaa mpango huo wa elimu, kwa niaba ya Kamishna wa Elimu wa Wizara ya Elimu, Mkurugenzi wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu iliyo nje ya Mfumo rasmi kutoka Wizara ya Elimu, Salum Mnjagila alisema mpango huo unatarajiwa kufanya kazi kwa kipindi cha miaka mitano kwa kuanzia mwaka 2017 – 2021 ili kuona ni jinsi gani utabadili elimu ya Tanzania.
Alisema kupitia kongamano hilo wanataraji kuchagua baadhi ya vipaumbele ambavyo wataona vinaumuhimu zaidi kuanza navyo kwa miaka mitano ya kwanza kwa mpango huo na baadae wataanza utekelezaji wa vipaumbele ambavyo vitakuwa vimepewa kipaumbele na washiriki wa kongamano hilo.
“Tupo hapa kufanya tathimini ya vipaumbele ambavyo vimeletwa mbele yetu ili tufanyie uchambuzi na tuone ni vipaumbele vipi tutaviweka kwenye mpango wa miaka mitano katika kuboresha sekta ya elimu nchini,” alisema Mnjagila.
Nae Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Makuru Petro ambaye ameshiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO alisema katika kuchambua elimu ya Tanzania wamegundua kuwa elimu imekuwa ikishuka na hilo linatokana na kuongezeka kwa wanafunzi wanaosajiliwa kuanza shule huku kukiwa hakuna maboresho ambayo yanafanyika ili kuboresha elimu hiyo.
Alisema baada ya uchambuzi kufanyika wanafanya tathmini ili kupata matokeo ambayo watajadili kwa pamoja kwa kushirikisha wadau mbalimbali kutoka mashirika ya kiserikali na yasiyo ya serikali ili kupitisha vipaumbele ambavyo vitafanyiwa kazi kati ya vipaumbele ambavyo wao waliwasilisha kwa washiriki hao.
“Elimu ya Tanzania hali sio nzuri tumefanya uchambuzi hata mashuleni hakuna hali nzuri mfano hata Geita tumekuta darasa moja linatumiwa na wanafunzi 80 hadi 100 na hilo ni tatizo na baada ya kuchambua changamoto na kuzifanyia tathmini tunazileta hapa ili tuchague vipaumbele vya kuanza kuvifanyia kazi,” alisema Petro.
Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kupitia kwa Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa shirika hilo nchini, Zulmira Rodrigues alisema lengo la kuweka mpango huo ni kuboresha elimu ya Tanzania kwa kuifanya kuwa bora na iliyo na usawa kwa makundi yote ya jamii kwa matokeo mazuri ya baadae.
Alisema kuna mambo ambayo yanatakiwa kupewa vipaumbele ikiwepo ni pamoja na ubora wa elimu, fursa za elimu kwa makundi yote katika jamii na kujenga uwezo kwa watendaji ambao wanatoa hiyo elimu kama ni walimu basi wawe wanapewa mafunzo kuendana na wakati uliopo ili kuwa na kitu kipya ambacho kinahitajika kwa wanafunzi kwa wakati huo.
IMG_1506
Mkuu wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini Ufaransa, Anton De Grauwe akiwasilisha vipengele mbalimbali vinavyotakiwa kujadiliwa na washiriki wa kongamano hilo katika kuandaa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021.
IMG_1683
Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akiwasilisha mambo mbalimbali muhimu yanayotakiwa kuzingatiwa kwenye Ajenda 2030 ya elimu na mpango wa utekelezaji katika kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).
IMG_1666

IMG_1683

IMG_1591
Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta (kushoto) akiteta jambo na Maofisa wenzake kutoka UNESCO, Faith Shayo (katikati) na Leonard Kisenha (kulia) wakati kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 likendelea.
IMG_1570
Mkurugenzi Msaidizi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Wizara ya Elimu, Bw. Makuru Petro ambaye akishiriki kufanya uchambuzi wa elimu ya Tanzania kwa kushirikiana na wataalamu kutoka UNESCO kwenye kongamano hilo.
IMG_1642
Mshauri wa Taasisi ya kimataifa ya mipango ya elimu (IIEP)/UNESCO, Barnaby Rooke akielekeza vipaumbele kwenye bajeti ya sekta ya elimu ambayo inahitaji maboresho makubwa ili kuleta mabadiliko kwenye sekta elimu nchini.
IMG_1596
Moja ya 'Papers' zilizowasilisha kwa washiriki.
IMG_1615
Mkurugenzi wa Sera na Mipango kutoka Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akishiriki kwenye kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) kwa mwaka 2017 - 2021 linalofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za NACTE jijini Dar es Salaam.
IMG_1738
Mwenyekiti wa Mtandao wa Redio za Jamii nchini (COMNETA), Joseph Sekiku akitoa maoni kuhusiana na udhaifu wa mipango ya sekta elimu nchini ambayo haitekelezeki wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP).
IMG_1784
Bi. Helena Reutersward, kutoka Ubalozi wa Sweden kitengo cha Elimu akitoa maoni wakati wa kongamano la kujadili Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu (ESDP) nchini linaloendelea katika ukumbi wa mikutano NACTE jijini Dar es Salaam.
IMG_1654
Pichani juu na chini ni wajumbe walioshiriki kongamano hilo kutoka taasisi mbalimbali za serikali, Wizara ya Elimu, Taasisi za Elimu na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
IMG_1539
IMG_1515

IMG_1533

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)