Pages

Nyota wa Leicester Vardy kufanyiwa upasuaji

Vardy
Mshambuliaji nyota wa Leicester City Jamie Vardy hataweza kucheza kwa wiki mbili baada yake kufanyiwa upasuaji.
Fowadi huyo wa Uingereza amefanyiwa upasuaji mdogo kwenye mtoki wake, kituo cha redio cha BBC cha Leicester kimeripoti.

Vardy amekuwa matata sana msimu huu na mabao yake 15 aliyoyafunga Ligi ya Premia yamesaidia Bweha hao kupanda hadi nambari mbili ligini.
Mchezaji huyo wa umri wa miaka 28 amechezea klabu hiyo mechi 24 msimu huu.

Vardy alicheza kwenye kikosi cha mkufunzi Roy Hodgson cha Uingereza kilichofuzu kwa michuano ya Euro 2016.

Alichezea klabu yake dakika zote 95 mechi dhidi ya Bournemouth ambayo walitoka sare ya 0-0 Jumamosi.

Kabla ya kujiunga na Leicester, Vardy alichezea klabu ya Fleetwood Town.Chanzo BBC Swahili

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)