Pages

MWENYEKITI WA BODABODA MKOA WA MWANZA AWAOMBA RADHI WATANZANIA.

Na"George Binagi-GB Pazzo @BMG

Mwenyekiti wa Waendesha Pikipiki (Bodaboda) Mkoa wa Mwanza Makoye Kayanda Bunoro anawatakia Waendesha Pikipiki wote nchini Kheri ya Mwaka Mpya 2016 huku akiwasihi kutimiza majukumu yao kwa kufuata sheria na taratibu za Usalama barabarani bila shuruti.

"Tuache Mchezo na Vyombo vya Moto, Tuvae Elmenti, tusibebe mishkaki (zaidi ya abiria mmoja) tusiendeshe kwa mwendo kasi kwani ni hatari, tusitumie pombe tukiwa kazini huku tikiwapenda abiria na kujiepusha na vitendo vya uhalifu vya aina yoyote". Anasema Bunoro.

Aidha Bunoro amewaomba radhi wale wote waliopata usumbufu kwa namna moja ama nyingine kutokana na kazi ya bodaboda na kwamba kusameheana ndilo jambo la msingi huku akiwakumbusha bodaboda  kujipanga katika majukumu yao ili kuendana na kasi ya Mhe.Rais Dkt.John Pombe Magufuli ya "Hapa Kazi Tu". Bonyeza HAPA Kusoma Zaidi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)