Pages

MGODI WA BUZWAGI WAISAIDIA MILIONI 10.5 TIMU YA AMBASSADOR FC - KAHAMA

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo  (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi katibu mkuu wa Ambassador FC, Bakari Khalid kwa  ajili ya maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa Shinyanga..

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (kushoto) na Bakari Khalid Katibu mkuu wa timu ya Ambassador wakati wa hafla ya kukabidhi msaada kwa timu hiyo.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhi hundi timu ya Ambassador FC.

Katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid akizungumza mara baada ya kukabidhiwa hundi na Uongozi wa Mgodi wa Buzwagi.

Baadhi ya wafanyakazi wa mgodi wa Buzwagi katika hafla ya makabidhiano ya hundi kwa timu ya Ambassador kwa ajili ya maandalizi ya ligi daraja la pili mkoa wa  Shinyanga.
Vikosi vya timu za Buzwagi fc na Ambassador vikiwa katika maandalizi wakati wa ukaguzi kabla ya kuanza kwa mhezo.
Kikosi cha timu ya Ambassador fc
Kikosi cha timu ya Buzwagi fc.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (mwenye kofia) akisalimiana na Nahodha wa timu ya Buzwagi, Saimon Sanga wakati wa mchezo wao wa kirafiki na timu ya Ambassador FC.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buzwagi Asa Mwaipopo (mwenye kofia) akisalimiana na wachezaji wa timu ya Ambassador FC.

Kikosi cha timu ya soka ya mgodi wa Buzwagi kikiwa katika picha ya pamoja wakati wa hafla ya kukabidhi hundi kwa timu ya Ambassador FC. Katika mchezo huo timu ya Ambassador FC iliibuka mshindi kwa kuwafunga wenyeji wao Buzwagi FC, 2-1
Kikosi cha wachezaji wa timu ya Ambassador FC ya mjini Kahama wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi na kampuni ya uchimbaji wa madini ya Acacia kupitia Mgodi wake wa Buzwagi ulioko wilayani Kahama.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mgodi wa dhahabu wa Buzwagi umeikabidhi timu ya ambassador FC ya wilayani Kahama kitita cha shilingi milioni kumi na laki tano kama sehemu ya msaada kwa ajili ya maandalizi ya kushiriki michuano ya ligi daraja la pili ngazi ya mkoa - Shinyanga.

Msaada huo ambao ulikabidhiwa na meneja mkuu wa Mgodi wa Buzwagi, Mhandisi Asa Mwaipopo umetolewa kwa timu hiyo ili kuiwezesha kufanya vizuri katika michuano ya ligi daraja la pili inayotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mfano wa hundi, meneja mkuu wa Buzwagi amesema msaada huo kwa timu ya ambassador ni mwendelezo wa harakati zinazofanywa na kampuni yake katika kuhakikisha makundi mbalimbali yanayozunguka maeneo ya mgodi huo yananufaika na fursa mbalimbali zilizopo.

“Lengo letu kubwa la kutoa msaada huu ni kutekeleza ahadi yetu ya kuisaidia Jamii inayotuzunguka na tungependa kuona hata kupitia michezo vijana wanajitengenezea ajira, kama mnakumbuka tumetoa udhamini kwa timu ya Stand Utd inayoshiriki Ligi kuu ya Vodacom na sasa tumetoa msaada huu wa fedha ili kuisaidia timu hii ili nayo iweze kufanya vizuri katika mashindano yaliyo mbele yao”.alisema Mwaipopo.

Kwa upande wake katibu wa timu ya Ambassador FC, Bakari Khalid ameushukuru uongozi wa mgodi wa Buzwagi kwa msaada huo ambao amesema utasaidia kuongeza hali ya mchezo kwa wachezaji wa timu yake.

“Natoa shukrani kwa uongozi wa Buzwagi kwa msaada huu, niwaahidi kwamba sisi kama Ambasador tutafanya vizuri nakuwa mabalozi wa kuitangaza Kahama katika sekta ya michezo, kwani tunao vijana wazuri wenye uwezo wa kucheza mpira na kwa kufanya hivi tunawahakikishia baadhi ya vijana ajira kupitia michezo” Alisema Bakari.


Katika hatua nyingine timu hiyo ya ambassador FC ambayo iko chini ya kocha Karume Songoro ambaye amewahi kuzichezea timu za Yanga na timu ya taifa ya Tanzania, ilimenyana na timu ya mpira ya Buzwagi mchezo ambao uliisha kwa Ambassador iliibuka na ushindi wa goli 2-1

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)