Pages

MGODI WA BULYANHULU WATOA ZAIDI YA MILIONI 300 KWA HALMASHAURI YA WILAYA YA NYANG'WALE KAMA USHURU WA HUDUMA.

Meneja Mkuu wa Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu Graham Crew akiwa na wafanyakazi wengine wa Bulyanhulu Gold Mine wakikabidhi mfano wa hundi kwa kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya Nyang'wale Venance Ngeleuya ,Wengine wanaoshuhudia tukio hilo ni Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Ibrahim Marwa .
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akiteta jambo na mkuu wa idara ya Mahusiano ya Jamii wa Mgodi huo Sara Terri wakati wa hafla ya kukabidhi hundi.
Madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wilaya ya Nyangwale Venance Ngeleuya akizungumza wakati wa makabidhiano ya hundi hiyo.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew akizungumza na baadhi ya viongozi na madiwani wa halmashauri ya Nyang’wale (hawapo pichani)wakati wa kukabidhi hundi kwa halmashauri hiyo.
Viongozi wa Mgodi wa Bulyanhulu  wakiwa kaika picha ya pamoja na Viongozi wa seriali pamoja na Halmashauri ya wilaya ya Nyang'wale.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

Mgodi wa dhahabu wa Bulyanhulu umekabidhi hundi yenye thamani ya Shilingi Milioni Mia Tatu Thelathini na Nne, Laki Sita na Elfu Themanini na Sita kwa Halamashauri ya Wilaya ya Nyang’wale.

Fedha hizo ni malipo ya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi ya mgodi huo kwa halmashauri ambapo Bulyanhulu inalipa kwa halamashauri ya Nyang’wale kutokana na makubaliano ya mwaka jana kwamba asilimia 35 ya malipo hayo yaende kwa wilaya hiyo na asimia nyingine kwa Halamashauri ya Msalala ambayo ndiyo mwenyeji wa Mgodi wa Bulyanhulu kwa asilimia kubwa.

Akipokea hundi hiyo Mkuu wa Wilaya ya Nyang’wale Mheshimiwa Ibrahim Marwa amesema, “Leo wenzetu wa Mgodi wa Bulyanhulu wamefunga safari kuja kutuletea hundi ya ushuru wa huduma kwa ajili ya halmashauri ya Nyangw’ale huo ni mwanzo mzuri, sasa tumepata chanzo kizuri cha mapato kutoka mgodi wa Bulyanhulu.”
“Lakini hiyo haitoshi tukijenga mahusiano vizuri watatusaidia zaidi, kuna eneo lao ambalo kuna wachimbaji wadogo wamevamia eneo hilo na baadhi ya viongozi wanawatetea, sasa ni lazima tuwe wa kweli kwenye mambo haya ya msingi, tunataka huku ushuru halafu huku tunataka kutetea wavamizi wa eneo lao ambalo wanalimiliki kwa leseni halali ya uchimbaji, hivi mtu akija nyumbani kwako akavamia akasingizia kwamba ana njaa ivi hiyo ni sababu.”
“Tutachukua hatua za juu ili tuwaondoe wale wachimbaji waliovamia katika kijiji cha mwasabuka wilaya ya Nyang’wale mkoani Geita”
Akizungumza baada ya kukabidhi hundi, Meneja Mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu Graham Crew amesema, “Ninashukuru sana kwa ushirikiano kutoka jamii na wilaya zinazozunguka mgodi wa Bulyanhulu, nashukuru pia kuona serikali ya awamu ya nne inahamasisha hapa kazi nafikiri hilo ni jambo zuri tuendelee kushirikiana ili kwa pamoja tulete maendeleo kwa taifa zima. Ijapokuwa bei ya dhahabu imeshuka lakini mgodi wetu wa Bulyanhulu bado umejidhatiti kuhakikisha kuchangia juhudi za maendeleo ya huduma za maendeleo ya jamii kadiri itakavyowekzekana.
Malipo ya ushuru wa huduma kwa kiwango cha asilimia 0.3 (0.3%) ya mapato ghafi ya mgodi yanafuatia makubaliano kati ya Serikali na Kampuni zinazomiliki migodi husika kufanya marekebisho kwenye Mikataba ya Maendeleo ya Uchimbaji Madini (Mining Development Agreement – MDA) baina ya Serikali na Migodi ikiwemo wa Bulyanhulu, kuhusu ulipaji wa ushuru wa 0.3% ya uzalishaji kulingana na Sheria ya Local Government Finance Act, Cap.290 Revised Editions of 2002 badala ya Dola za Marekani 200,000 kwa mwaka zilizokuwa zikilipwa awali

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)