Pages

JANET MWENDA NA MARAFIKI ZAKE WA "MENTORING AND NETWORKING" WATOA MSAADA KWA KITUO CHA WATOTO WETU TANZANIA

Picha No 1
Bi. Janet Sosthenes Mwenda (wa pili kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete moja ya vitu vilivyowasilishwa kwenye kituo hicho ndoo ya sabuni ya unga. Kushoto ni Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga na wengine wanaoshuhudia ni watoto wa kituo hicho. (Picha zote na Andrew Chale, Modewjiblog).

Na Andrew Chale, Modewjiblog
[DAR ES SALAAM] Mmiliki na Mwendeshaji wa kipindi cha ‘Ongea na Janet’ Bi. Janet Sosthenes Mwenda ambaye pia ni mmiliki wa programu maalum ya vipindi vya watoto katika kutoa elimu katika televisheni kiitwacho ‘Tuwalinde Watoto Wetu’ kwa kushirikiana na marafiki zake wa kundi la “Mentoring and Networking” kupitia mitandao ya kijamii wametoa misaada mbalimbali ya vyakula na vinywaji kwa kituo cha Watoto Wetu Tanzania.
Akizungumza wakati wa kutoa misaada hiyo mapema jana 17 Januari, wakati wa tukio hilo lililofanyika kwenye kituo hicho kilichopo Kimara jijini Dar es Salaam, Janet Mwenda ambaye aliambatana na baadhi ya marafiki zake hao wa “Mentoring and Networking” wameweza kutoa misaada hiyo ya vyakula, vinywaji ambavyo vitasaidia kituo hicho.

“Kwa kuja hapa kutoa msaada huu ni kutokana na kuguswa na hali ya watoto wanaolelewa hapa na kwingineko kote. Naamini msaada huu utasaidia watoto wetu hapa kituoni naamini kwa hiki kidogo kitasaidia kwa siku kadhaa” alieleza Janet Mwenda.

Janet Mwenda ameongeza kuwa, amekuwa akifikiria zaidi kutoa misaada hivyo kufika hapo ni kutokana na kuguswa kwake kwa muda mrefu na amekuwa pia akitembelea kituo hicho kipindi cha nyuma hivyo kuwa miongoni mwa wanafamilia.

Kwa upande wake Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga ambaye aliambatana na Janet Mwenda katika kituo hicho ametoa wito kwa jamii kujitokeza kusaidia watoto wanaolelewa kwenye vituo kama hivyo na kuchangia chochote walicho nacho.
Pia amepongeza watu mbalimbali kwa kuguswa na hali ya watoto wanaolelewa kwenye vituo hivyo ameomba waendelee kujitokeza zaidi pindi wanapoguswa na masuala ya kusaidia jamii isiyo jiweza.

Naye Mkurugenzi wa kituo hicho, Ndugu Evans Tegete akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea msaada huo ambapo alishukuru kwa kuguswa kwa Janet Mwenda na marafiki zake kwani hadi sasa kituo hicho hakina Mfadhili wa kudumu zaidi wakitegemea kuendesha kituo kwa michango ya misaada ya watu mbalimbali wanaofika kituoni hapo.
“Tunashukuru kwa msaada huu. Kwani ni mkubwa sana na utasaidia kuendesha kwa siku kadhaa ndani ya kituo chetu. Kituo chetu kwa sasa tuna watoto na vijana zaidi ya 89 wakiwemo wale wanaosoma shule za Bweni na wa kutwa ambao wapo hapa kituoni.” Alieleza Mkurugenzi huyo.
Pia alieleza kuwa changamoto mbalimbali zinawakabili ikiwemo suala la ada za shule kwa watoto na vijana waliochini ya kituo hicho.

Kituo hicho kinacholea Watoto na vijana wa mitaani na wanaoishi katika mazingira magumu kina jumla ya watoto pamoja na vijana 120 kilianzishwa mnamo mwaka 1998 Kwa lengo la kuwasaidia watoto waliokosa malezi na huduma mbalimbali za kijamii. Kituo hicho kinapatikana Kimara Suka pamoja na Kijiji cha Mazizini Msata wilayani Bagamaoyo kinakabiliwa na changamoto mbalimbali hivyo uongozi wa kituo hicho kinawaomba watu binafsi na wafadhili mbalimbali kujitokeza kuwasaidia pindi waguswapo.
Picha No 2
Mkurugenzi wa kituo cha Watoto Wetu Tanzania, Bw. Evans Tegete akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) wakati wa utambulisho wa kituo hicho.
Picha No 3
Bi. Janet Sosthenes Mwenda (kushoto) akipata fursa ya kuwa na watoto wanaolelewa kwenye kituo hocho cha Watoto Wetu Tanzania, kulia kwake ni Mary Sanga kutoka kundi la marafiki wa “Mentoring and Networking”.
Picha No 4
Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga akitoa nasaha na kushukuru wale wote walioguswa kwa kuchangia mpango huo.
Picha No 5
Bi. Janet Sosthenes Mwenda akipata fursa ya kuwa na watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania.
Picha No 6
Bi. Janet Sosthenes Mwenda akizungumza na wanahabari (hawapo pichani) ambapo ameiomba jamii kuwa na tabia ya kusaidia jamii isiyojiweza ikiwemo watoto wanaolelewa kwenye vituo.
Picha No 7
Binti Cecilia Sospita anayelelewa kwenye kituo hicho cha Watoto Wetu Tanzania, akishukuru kwa niaba ya watoto wenzake wanaolelewa kituoni hapo kwa msaada uliowasilishwa na Bi. Janet Mwenda.
Picha No 8
Msaada uliotolewa kusaidia kituoni hapo.
Picha No 9
Kijana Samson Furgence akishukuru kwa niaba ya watoto wenzake wa kituo hicho.
Picha No 10
Zoezi la utoaji wa zawadi likiendelea.
picha no 11
Watoto na vijana wanaolelewa katika kituo hicho. Wengine ni wageni wa kujitolea "Volunteer" wa kituo hicho kutoka nchini Ujerumani wakiwa pamoja na watoto hao kituoni hapo.
Picha No 12
Muhamasishaji na mchangishaji fedha wa “Mentoring and Networking”, Bi. Mary Sanga akitoa msaada katika tukio hilo.
Picha No 14
Baadhi ya watoto na walezi wao wakifuatilia shughuli hiyo.
picha no 16
Janet Mwenda akishukuru watu mbalimbali kwa kumtia moyo katika kufanikisha shughuli hiyo.
picha no 17
Baadhi ya watoto hao.
picha no 18
Baadhi ya watoto hao.
picha no 19
Sala maalum ya kuombea vitu hivyo vilivyoletwa kituoni hapo pamoja na Baraka kwa waliofanikisha ikitolea na mmoja wa watoto wa kituo hicho.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)