Pages

Inspekta Prisca awapiga msasa wa somo la jinsia wafanyakazi wa TBL wa Arusha na Moshi

 Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni, Inspekta Prisca Komba akitoa mada wakati wa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL yaliyofanyika mjini Moshi leo .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini.
 Mfanyakazi wa Kiwanda cha Tanzania Breweries Limited kilichopo  mjini Moshi, Siraji Muya, akichangia mada wakati wa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL yaliyofanyika mjini Moshi leo .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini.
Mfanyakazi wa Kiwanda cha TBL cha mjini Moshi Venance Mwakosya  akichangia mada wakati wa mafunzo ya jinsia kwa wafanyakazi wa kiwanda cha TBL yaliyofanyika mjini Moshi leo .Mafunzo haya yanaendelea katika viwanda vyote vilivyopo chini ya TBL Group nchini.

Wafanyakazi wa kampuni ya TBL Group wanaofanyika kazi katika kiwanda cha kutengeneza bia cha bia cha Arusha na Moshi wamepata fursa ya kupatiwa  elimu ya  jinsia kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa jeshi la Polisi wa Dawati la Jinsia wilaya ya Kinondoni, Inspekta Prisca Komba.

Baadhi ya wafanyakazi hao kwa nyakati tofauti wameeleza kuwa wameweza kujua mengi kuhusiana na suala la jinsia kwa ujumla na kupata fursa za kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na jinsia.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)