Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi Suleiman S. Suleiman.
SALAMU ZA RAMBIRAMBI
Dar es Salaam, 19 Januari, 2016
Uongozi na wafanyakazi wa Fastjet Tanzania umepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha ghafla cha Mkurugenzi Mkuu wa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania, hayati Mhandisi Suleiman S. Suleiman.
Tunaungana na familia, marafiki, ndugu, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kutuma salamu za rambirambi katika kipindi hiki cha kuomboleza.
Fastjet Tanzania imefanyakazi kwa ukaribu na Mhandisi Suleiman na tunatambua mchango wake katika kukuza sekta ya usafiri wa anga nchini.
Tutaukosa kwa kiwango kikubwa ushauri, uongozi na ushauri wake kutokana na kifo chake.
Tunaomba roho yake ipumzike kwa amani peponi.
Amin.
Imetolewa na Meneja Mkuu wa fastjet
Tanzania, John Corse.
|
No comments:
Post a Comment
Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)