Pages

DK. KIGWANGALLA AFANYA ZIARA MUHIMBILI NA KUKAGUA MASHINE ZA CT-SCAN NA MRI, AFURAHISHWA NA UTENDAJI KAZI

IMG_0833
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Rabi Hume, Modewjiblog
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla amefanya ziara, Januari 4, 2016 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kutembelea idara mbalimbali za hospitali hiyo kuona jinsi ya ufanyaji kazi.
Baadhi ya idara ambazo, Dk. Kingwangalla alitembelea ni pamoja na Kitengo cha dharura, Chumba cha wagonjwa Mahututi (ICU), wodi ya Mwaisela, duka la dawa la MSD na kukagua ufanyaji wa kazi wa mashine ya CT-Scan na MRI.

Akizungumzia ziara hiyo mara baada ya kutembelea Hospitalini hapo, Dk. Kigwangalla ameeleza kuwa ili kuweza kuona hali ya utendaji wa kazi iliyopo katika hospitali hiyo ya taifa tangu ambapo Rais, Dkt. John Pombe Magufuli alipofanya ziara ya kushtukiza na kutokuridhishwa na utendaji kazi wa hospitali hiyo hali iliyopelekea kuivunja bodi iliyokuwa ikisimamia hospitali.

Dk. Kingwangalla alisema amefurahishwa na utoaji wa huduma katika upimaji kwa kutumia mashine ya CT-Scan na MRI ambazo awali wakati wanaingia madarakani hazikuwa katika hali nzuri ya ufanyaji wa kazi na kuwataka watumishi wa hospitali hiyo kufanya kazi kwa bidii na kuifanya hospitali hiyo kuonekana yenye hadhi ya kuwa hospitali ya taifa.

Alisema limekuwa jambo ambalo linasikitisha kuona huduma zinazopatikana katika hospitali ya taifa zinashindwa na huduma zinazotolewa katika hospitali za watu binafsi na akilinganisha huduma za kulipia vitanda zinazotolewa Muhimbili kuwa hazina viwango vya juu ambavyo vinaweza kuwashawishi wananchi wenye uwezo kuacha kwenda hospitali binafsi na kwenda hospitalini hapo.
“Ni jambo la kushangaza hospitali za watu binafsi zinakuwa na watu wengi kuliko hapa na wakati sisi tuna madaktari bingwa zaidi ya 500 hapa Muhimbili lakini hizo hospitali zao hazina hata daktari mmoja bingwa lakini na huduma zinazopatikana katika madaraja ya juu zinatakiwa kuboreshwa,

“Kama tunaweza kuwa na huduma nzuri katika first class (daraja la kwanza) tunaweza kuwavuta wananchi wengi waje hapa na waache kwenda hospitali binafsi, wanatakiwa kutengwa madaraja ya juu ambayo huduma zake zinakuwa zimeboreshwa sio mtu anakuwa daraja la kwanza alafu bado anachangia choo na wengine au anaelala nae hapewi kitanda,” alisema Mhe. Kingwangalla.
Aidha Mhe. Dkt.Kingwangalla aliwatupia lawama Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kwa jinsi wanavyopanga madaraja ya hospitali na kuilinganisha Muhimbili na hospitali zingine za watu binafsi kuwa jambo hilo siyo sahihi kwa kuiweka hospitali ya taifa sawa na hospitali za watu binafsi.

“NHIF wanaweka sehemu moja hospitali ya taifa na hospitali binafsi hili haliwezekani walinganishe huduma zilizopo hospitali ya taifa na zile zingine, nina mpango wa kuwatembelea hivi karibuni nitazungumza nao,” alisema Kingwangalla.

Aidha Mhe. Naibu Waziri aliupongeza uongozi wa hospitali hiyo kwa kuongeza vitanda katika wodi ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo awali ilikuwa na vitanda sita hali ambayo ilikuwa ikiwashangaza wananchi wengi kutokana na kuwepo kwa vitanda zaidi ya 1350 katika hospitali hiyo na hivyo kuongezeka kwa vitanda katika wodi hiyo kutasaidia upatikanaji wa wa huduma bora kwa wagonjwa wanaofika hospitalini hapo kupata huduma.

Awali akitoa taarifa mbele ya Mhe. Dkt. Kingwangalla, Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali hiyo, Dkt. Flora Rwakatare alisema tangu kuanza kwa kutumika kwa mashine ya MRI mwishoni kwa mwezi Novemba mwaka jana jumla ya wagonjwa 560 wamefanyiwa vipimo katika mashine hiyo na ndani ya siku tatu amabazo wamefunga mashine mpya ya CT-Scan wameshawapima wagonjwa 26.

Alisema kufungwa kwa mashine ya CT-Scan kunaonekana kuwepo kwa matumaini mapya kwa watanzania kutokana na kasi ya ufanyaji kazi kwa mashine hiyo ambayo imetengenezwa na kampuni ya Siemens ambayo inauwezo wa kupima kifua na tumbo kwa sekunde 6.

“Mashine ya CT-Scan ambayo imefungwa ina ubora mkubwa na ni ya pili kwa ukubwa Afrika Mashariki na kwasasa tunategemea kufanya kazi kwa ubora zaidi kutokana na ukubwa iliyonayo na inaweza kufanya kazi kwa kasi tofauti na ile iliyokuwa ikitumika awali,” alisema Dkt. Flora.
Nae Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru alisema awali hawakuwa wakifanya visingizo ili wasifanye kazi lakini ni hali halisi iliyokuwepo kuwa mashine iliyokuwepo awali ilikuwa na matatizo lakini kufanikisha kufungwa kwa mashine mpya ambayo imeigharimu serikali Dola za Kimarekani Milioni 1.7 ambapo ni zaidi ya Milioni 400 za kitanzania kutawapa wao motisha ya kufanya kazi kwa kutumia kifaa cha kisasa na chenye kufanya kazi kwa haraka.
IMG_0836
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akitoka katika ofisi ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali hiyo.
IMG_0857
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akisalimiana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto). Katikati ni Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0861
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiongozana na Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) pamoja na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga (kulia) kuelekea kwenye chumba cha vipimo vya CT Scan pamoja na MRI alipofanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo, Januari 4, 2016.
IMG_0873
Baadhi ya watumishi katika kitengo cha vipimo cha MRI wakiandaa kitanda kwa ajili ya kumpokea mgonjwa wa kipimo cha MRI (hayupo pichani) kama walivyokutwa na mpiga picha wa wetu.
IMG_0876
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata taarifa ya idadi ya wagonjwa waliofanyiwa vipimo tangu mashine hiyo ipone kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare (kulia).
IMG_0886
Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare akizungumza jambo na waandishi wa habari katika chumba cha vipimo vya MRI wakati wa ziara ya kushtukiza iliyofanywa na Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla, Januari 4, 2016.
IMG_0891
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa ndani ya chumba cha vipimo vya MRI katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili ya jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kushtukiza, Januari 4, 2016.
IMG_0900
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akipata maelezo ya mashine mpya ya CT Scan iliyonunuliwa hivi karibu na Serikali kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0903
Kaimu Mkurugenzi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru (kushoto) akitoa maelezo ya uwezo mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibuni ambayo hadi kufikia Januari 4, 2016 ikiwa na muda wa siku tatu tangu kuanza kutumika hospitalini hapo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla.
IMG_0910
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akimpongeza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru baada ya kuona mabadiliko makubwa katika hospitali hiyo tangu alipokaimu kiti hicho wakati wa zaiara ya kushtukiza katika chumba kilichofungwa mashine mpya ya CT-Scan iliyonunuliwa na Serikali hivi karibu na inauwezo mkubwa wa kufanya kipimo kwa sekunde 6 na kutoa majibu. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mionzi katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Flora Rwakatare.
IMG_0924
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla akiwa kwenye dirisha la malipo ya matibabu hospitalini hapo wakati wa ziara ya kushtukiza aliyoifanya, Januari 4, 2016.
IMG_0930
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dk. Hamisi Kingwangalla aliyetembelea kitengo chake, Januari 4, 2016. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru.
IMG_0932
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akiendelea kupewa maelezo ya namna wananchi wanavyohudumiwa katika kitengo hicho na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinanga.
IMG_0935
Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Dharura na Ajali ambaye pia ni daktari bingwa wa magonjwa ya dharura katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dkt. Juma Mfinangaakitoa maelezo ya ubao maalum unaowaongoza madaktari na wagonjwa wanaohudumiwa katika kitengo hicho kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla.
IMG_0950
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe.Dk. Hamisi Kingwangalla akikagua wodi mpya ya wagonjwa mahututi (ICU) ambayo ipo kwenye hatua za mwisho kukamilika. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Prof. Lawrence Mseru akimtembeza Mh. Naibu Waziri kwenye wodi hiyo.
IMG_0951

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)