Pages

BALOZI WA NORWAY NCHINI ATEMBELEA MRADI WA KUFUA UMEME KATIKA KITUO CHA KIKULETWA WILAYANI HAI.

Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na balozi wa Norway nchini Tanzania Hanne-Marie Kaarstad wakati akimpokea ofisini kwake kwa ajili ya ziara ya kutembelea kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akisalimiana na Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha,(Arusha Techinical) Dkt Richard Masika aliyeongozana na balozi wa Norway katika ziara ya kutembelea kituo cha kufulia umeme cha Kikuletwa.
DC Mtaka akiongozana na Balozi Kaarstad kuelekea ofisini kwake.
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha ,Dkt Richard Masika akiteta jambo na Balozi wa Norway Kaarstad ofisini kwa mkuu wa wilaya ya Hai.
Mkuu wa wilaya ya Hai ,Anthony Mtaka akizungumza na ugeni wa balozi wa Norway ofisini kwake .
Baloozi Kaarstad akimueleza jambo DC Mtaka.
Ugeni wa Balozi wa Norway ukiwa umetembelea kivutio cha Utalii cha Chemka ambako kuna Chemichemi ya maji yenye uvuguvugu ambako watalii wamekuwa wakitembelea na kuogelea.
Kivutio cha Utalii cha Chemka ambacho maji yake yanatokana na Chemichemi .
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha ambao ndio waendeshaji wa kituo cha kufulia umeme cha Kikuletwa  akitoa maelezo kuhusu mradi wa ukarabati mkubwa uanaotaraji kufanywa kwa msaada wa serikali ya Norway.
Mooja ya mioundo mbinu katika kituo cha kufulia umeme cha Kikuletwa.
Balozi Kaarstad akiongozwa kutembelea maeneo mbalimbali katika kituo cha Kufulia umeme cha Kikuletwa.
Sehemu ya Mitambo ya kufua umeme katika kituo cha Kikuletwa inavyoonekana kwa sasa baada ya kukaa kwa muda mrefu bila kufanya kazi.
Mkuu wa wilaya ya Hai,Anthony Mtaka akizungumza jambo na Mkurugenzi mkuu wa Tume ya Nguvu za Atomiki Profesa Idd Mkilaha walipkutana wakati wa kutembelea Kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Ugeni wa Balozi wa Norway Kaarstad ukitembelea maeneo mbalimbali ya mradi huo .
Mkurugenzi wa Chuo cha Ufundi cha Arusha,Dkt Masika akimuonesha Balozi Kaarstad mfereji mkuu wa kupeleka maji katika kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Kazi ya uondoaji tope ikiendelea katika mfereji huo.
Sehemu ya maporomoko ya maji yanayotiririka katika mto Kikuletwa.
Balozi wa Norway ,Henne-Marie Kaarstad akizungumza na wanahabari katika eneo ambalo maji yanapita kwa kasi katika mto Kikuletwa.
Ugeni wa Balozi wa Norway ukitizama moja ya mito inayotirisha maji kuelekea katika kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
Mto unaotenganisha wilaya ya HAi na Simanjro mkoani Manyara unaopeleka maji katika kituo cha kufua umeme cha Kikuletwa.
DC Mtaka akimuongoza balozi Kaarstad kupita katika moja ya daraja lilopo eneo la mradi . Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)