Pages

BALOZI NYANG'ANYI AHANI MSIBA WA LETICIA NYERERE LANHAM, MARYLAND

 Balozi Mustafa Nyang'anyi akiwa na Bw. Madaraka Nyerere alipokwenda kutoa pole kwa msiba wa Leticia Nyerere siku ya Jumanne January 12, 2016 Lanham, Maryland. Maarehemu Leticia Nyerere aliaga Dunia siku ya Jumapili January 10, 2016 katika Hospitali ya Jumuiya ya Madaktari( Doctors Community Hospital) iliyopo Lanham, Maryland. Mwili wa mpendwa wetu utasafirishwa kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi baada ya taratibu zote kukamilika. Kwa wanaDMV siku ya misa ya kumbukumbu na kumuaga mama yetu tutataarifiwa pindi mipango yote itakapokamilika na mazishi yanatarajiwa kufanyika Butiama.

Ndugu, Jamaa na marafiki wakiwa nyumbani kwa marehemu, Lanham, Maryland kutoa pole kwa wafiwa.Msiba upo 9004 brightlea court, Lanham MD 20706.Kama mila na desturi zetu tufike kuwafariji familia. Kwa maelezo zaidi wasiliana na : Margareth mageni 240 462 9138 Emmanuel muganda 240 447 2801 Ramadhani kamguna 202 459 3839

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)