Pages

WAZIRI WA AFYA NA NAIBU WAKE WAJITAMBULISHA KWA WAFANYAKAZI

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu(kulia), akizungumza na wafanyakazi wa sekta ya Afya wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo ambao
ulikwenda sanjari na kujitambulisha na Naibu wake,Dk.  Hamisi Kigwangala
baada ya kuteuliwa na Rais kushika nafasi hiyo uliofanyika Dar es Salaam
leo asubuhi. Kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Mery Ntira na katikati ni Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk.Hamisi Kigwangala.
Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk.Hamisi Kigwangala (katikati), akijitambulisha mbele ya Baraza hilo. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Donan Mmbando.
Kushoto ni mtoa mada katika Baraza hilo, Dk. Neema Rusibamayila na kulia ni Kaimu Kamishna Ustawi wa Jamii, Rabikira Mushi.
Mkuu wa Kitengo cha Tehama (ICT) wa Wizara hiyo, Hermes Rulagirwa (kulia) na Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Bernard Konga wakiwa kwenye mkutano huo.
Wajumbe wa baraza hilo wakimsikiliza Waziri Ummy wakati akifungua baraza hilo.
Wajumbe wa baraza hilo wakimsikiliza Waziri Ummy wakati akifungua baraza hilo la siku moja.
 Baraza likifunguliwa.

Na Dotto Mwaibale

WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amewataka wafanyakazi wa wizara hiyo kuchapa kazi kwa bidii ili kwenda sanjari na kauli mbiu ya Rais Dk.John Magufuli ya Hapa ni Kazi tu kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Ummy alitoa mwito huo wakati akifungua mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo ambao ulikwenda sanjari na kujitambulisha na Naibu wake, Hamisi Kigwangala baada ya kuteuliwa na Rais kushika nafasi hiyo uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi.

"Kwanza tunamshukuru Rais Dk. John Magufuli ya kuwa na imani na sisi ya kututeua kuwa mawaziri wa kuongoza wizara hii nikiwa na mwenzangu Daktari mwenzenu Hamisi Kigwangala ambapo naamini tutashirikiana vizuri katika kuwa hudumia wananchi" alisema Mwalimu.

Mwalimu alisema kuwa kazi iliyopo mbele yao sio kubwa bali ni nyepesi iwapo tu utakuwepo ushirikiano baina yao na wafanyakazi wote kwa ujumla wa sekta ya afya nchini.

Aliwataka wafanyakazi wa sekta hiyo kila mmoja wao mahali alipo kufanya kazi kwa bidii na kuacha kuwa waoga mbele yao kwani lengo lao kubwa ni kufanya kazi kwa ufanisi na si kuogopana.

Aliwataka wafanyakazi hao kufanya kazi kwa uwazi, uadilifu na uchapakazi ili kuwatumikia wananchi ambao wanahitahi kupata huduma bora kutoka kwako badala ya bora huduma.

Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Donan Mmbando alisema Tanzania ni moja ya nchi 89 ambazo zilikubali kutekeleza malengo nane hadi kufikia mwaka 2015 na kuwa katika lengo namba nne Tanzania tayari imefikia lengo la kupunguza vifo vya watoto wadogo.

Dk.Mmbando alisema hali hiyo imetokana na jitihada za wafanyakazi na kuweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kupunguza vifo hivyo ambapo aliongeza kuwa mbali na mafanikio hayo bado kunachangamoto kubwa sana ya kupunguza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua.

Alisema lengo namba sita nalo wameenda vizuri ambalo linaendana na magonjwa makubwa manne yaani Ukimwi, Kifua Kikuu (TB) na Malaria na kuwa Tanzania imefikia lengo la kutokomeza ukoma ambapo waliwekewa lengo la mgonjwa mmoja kwa watu elfu kumi.

Alisema malengo hayo yasingeweza kufikiwa bila ya jitihada za wajumbe ambao ndio nguzo ya huduma za Afya na Ustawi wa Jamii nchini.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)