Pages

WALIOSOMA HOGONGO SEKONDARY WILAYANI MUHEZA MKOANI TANGA WAKUTANA KUUNDA CHAMA CHA KUSAIDIANA

Mwenyekiti wa muda wa wanafunzi waliosoma Shule ya Sekondari ya Hogongo iliyopo Muheza mkoani Tanga, Elliude Pemba (kulia), akizungumza na wanafunzi wenzake wa shule 

hiyo waliosoma kuanzia 1980 hadi 1990 wakati wakijadili mchakato wa kuunda chama chao cha kusaidiana  na kuisaidia shule hiyo kilichofanyika Sinza Dar es Salaam jana. 
Mmoja wa wanafunzi hao, Felix Sesod 'Bibo' akichangia jambo kwenye mkutano huo.
Mwanafunzi mwingine wa shule hiyo wa miaka hiyo, Nasir Seif Mohamed (katikati), akichangia jambo.
Nora Muya (kushoto), naye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa shule hiyo wa wakati huo akichangia jambo. Kulia ni Mossi Kombo.

Na Dotto MwaibaleWANAFUNZI wa zamani wa Shule ya Sekondari ya Hogongo iliyopo wilayani Muheza mkoani Tanga wamekutana jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuunda umoja ili wawe na nguvu moja ya kusaidia shule hiyo katika maeneo tofauti.

Akizungumza katika mkutano uliowakutanisha wanafunzi hao Dar es Salaam juzi, Mwenyekiti wa muda wa mkutano huo Elliude Pemba alisema ni muhimu kwa wao kuikumbuka shule hiyo kwa kuisaidia.

"Sisi wanafunzi tuliosoma katika shule hiyo kuanzia 1980 hadi 1990 tumeona kuna umuhimu wa kuanzisha chama chetu ilituweze kuwa pamoja na kuisaidia shule iliyotupatia elimu" alisema Pemba.

Alisema maeneo ambayo wameona kuna nia ya kuisaidia shule hiyo ni ukarabati wa majengo, maktaba na miundombinu mbalimbali ili kutoa fursa kwa wanafunzi kupata eneo zuri la kupata elimu.

Pemba aliongeza kuwa eneo lingine ambalo wataisaidia shule hiyo ni pamoja na vifaa vya michezo na mchakato huo utafanyika baada ya kukutana wote na kujiwekea mikakati mbalimbali.

Alitumia fursa hiyo kuwaomba wanafunzi wote waliosoma katika shule ambao wapo nje ya Dar es Salaam kuwasiliana nao ili kukamilisha mchakato wa chama hicho na kujua idadi yao jambo litakalosaidia kurahisisha mpango huo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)