Pages

Updates za dada Joyce Richard Mwambepo wa mbeya aliyelazwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kuvunjika miguu ajalini

Ankal akiwa wodini kumtembelea dada Joyce 
 Dada Joyce alipowasili Hospitali ya Taifa ya Muhimbili wiki iliyopita
Dada Joyce akiwa wodini MOI


Ndugu Wasamaria Wema,

Tunapenda kutumia fursa hii kuwashirikisha tena habari ya kusikitisha kuhusu dada Joyce Rishard Mwambepo (pichani akiwa na mwanaye wa miaka 4, na miguu yake iliyopooza) mkaazi wa Sinde jijini Mbeya. Dada huyu mwenye umri wa miaka 27 anaishi na bibi yake mwenye umri wa miaka 80 pamoja na huyo mwanaye wa miaka 4.
Kwa bahati mbaya mwezi April mwaka jana wa 2014 dada huyu alipata ajali ya kugongwa na gari ambayo dereva hakusimama kumsaidia. Ila kwa msaada wa wasamaria wema alipelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa  Mbeya ambako alikaa kwa miezi mitatu bila kupata matibabu, kwa kukosekana nyenzo pamoja na pesa  za kumfanyia uchunguzi.
Katika uchunguzi wa awali ilibainika kuwa Joyce amevunjika miguu yote miwili,  hivyo akahamishiwa katika hospitali ya Taifa Muhimbili ambako pia baada ya kukaa kwa miezi kadhaa alirejeshwa tena Mbeya baada ya kukosa pesa  za vipimo na matibabu.
Hadi  Msamaria mwema na Mpiganaji Deo Kakuru anakutana naye dada huyu alikuwa amelala nyumbani kwa bibi yake ambaye ni mlezi wake tangu akiwa na miaka minne baada ya wazazi wake wote wawili kufariki dunia. 

Hawezi kukaa wala kusimama na anajisaidia hapo hapo kitandani kwa msaada wa mwanaye huyp na bibi yake.  Inasikitisha.
Hivyo Deo Kakuru, kwa msaada mkuwa wa michango ya Wasamaria Wema,  amefanikiwa kumsafirisha dada Joyce kwa Fast Jet kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mbeya  hadi Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kitengo cha MOI jijini Dar es salaam ambako alipokelewa na kulazwa katika jengo jipya liitwalo Wodi ya Magufuli ghorofa ya tatu wodi namba 2.
--------------------------------------
UPDATES:

Baada ya Deo Kakuru kuweka mitandano tatizo la dad Joyce, Wasamaria Wema kadhaa wakajitokeza kumsaidia.  Hatuna uhakika kwamba wote wangependa majina yao yawekwe hadharani, Ila tunapenda hadi sasa kukiri upokeaji wa Tshs:

1. 505,000/-

2. 50,000/-

3.100,270/-

4. 10,000/-

5. 100,000/-

6. 500,000/- (ahadi ya uhakika)

7. 500,000/- (Michuzi Media Group)

7. 800,000/-  (Kulipia gharama za vipimo vya CT Scan Regency Hospital mgonjwa atapofikishwa Dar es salaam).


Hivyo ndiyo kusema jumla ya Tshs. 2,565,270/-  tayari zilikusanywa kumsaidia dada yetu huyu anayeteseka. Kwa niaba ya mgonjwa tunashukuru sana kwa msaada huo, hana cha kuwalipa zaidi ya kuwaombea kwa Mola mzidishiwe pale mlipopungukiwa. KUTOA NI MOYO.


Aidha, kwa kiasi kilichopatikana tayari dada Joyce ameshafanyiwa vipimo vya MRI  Alhamisi  iliyopita na hivi sasa yanasubiriwa majibu siku ya Jumatatu ambapo baadaye Jopo la Madaktari Bingwa litaka na kuamua nini kifanyike kimatibabu. Tunashukuru madaktari na watumishi wote wa MOI kwa kuhitimisha hilo, nasi tunaendelea kuwaomba waendelee na huduma hiyo hadi dada Joyce atapopata matibabu.

Vile vile tunamshukuru sana Msamaria Mwema Mama Rozi aliyejitolea kumhudumia dada Joyce pale wodini ambako mama yake mzazi amelazwa na ana matatizo karibu sawa na ya dada yetu. Bila kuchoka mama Rozi amekuwa akimletea chakula na vinywaji dada Joyce kila siku na kumfanyia huduma za usafi kila siku. Ubarikiwe sana Mama Rozi.

Shukurani pia ziwaendee wasamaria wema wengine pamoja na wadau ambao baada ya kuguswa na matatizo ya dada Joyce wamekuwa wakimtembelea hapo wodini na kumfariji. Asanteni sana.


Wito wetu tunaomba tuendelee kumsaidia kwa hali na mali dada Joyce kwani mara baada ya majibu ya vipimo yatapotoka Jumatatu, ni dhahiri kutakuwa na mahitaji zaidi katika matibabu yake. 


Wakati huo huo kwa niaba ya Michuzi Media Group, Ankal anaendelea kusaidia uratibu wa kufanikisha matibabu ya dada Joyce akiwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Kitengo cha MOI. Hivyo unaweza kuwasiliana naye kwa email issamichuzi@gmail.com ama whatsapp namba+255 754 271266 kwa jina la Ankal.

Mratibu mwenza Deo Kakuru naye anaendelea kusaidia kwa kumtunza bibi yake Joyce na mwanae mwenye umri wa miaka 4 huko Mbeya.

Deo Kakuru Msimu
Msamaria mwema

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)