Pages

UNESCO YAZINDUA RIPOTI YA MAFANIKIO YA MRADI WA WAZAZI MATINEJA

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues akisoma hotuba mbele ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa Ripoti ya Mafanikio ya Mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.(Picha zote na Geofrey Adroph wa Pamoja blog)
Kamishana wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi nchini Prof, Eustella Bhalalusesa akizungumza jambo pamoja na kuwashukuru wadau ambao ni hirika la Umoja wa Mataifa linalohudumia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) pamoja Ubalozi wa Japani nchini Tanzania ambao wamefanikisha mradi huo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya mafanikio ya mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.

Balozi wa Japani nchini Tanzania Mh. Masaharu Yoshida akisoma hotuba yake wakati wa uzinduzi wa Ripoti ya mafanikio ya mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito uliofadhiliwa Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO Tanzania.
Mshauri na Mwakilishi kutoka shirika la UNFPA, Anna Holmstrom akitoa ufafanuzi wa ripoti iliyofanyika katika mkoa wa Shinyanga juu ya wazazi wenye umri mdogo waliopta mimba wakiwa bado shuleni.

Ofisa mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta ambaye alikuwa ni msimamizi wa mradi akitolea ufafanuzi kuhusu mradi huo ikihusisha changamoto pamoja na faida za mradi huo uliofanyika Mkoani Shinyanga.

Baadhi ya wageni waliofika katika uzinduzi wa Ripoti ya mafanikio ya mradi wa Wasichana walioacha shule kwa sababu za Ujauzito unaofadhili Ubalozi wa Japan na kuratibiwa na UNESCO.

Katibu Tawala wa mkoa Shinyanga, Bw. Abdul Rashid Dachi akizungumza jambo wakati wa uzinduzi huo wa ripoti hiyo.

Mkuu wa ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues (kushoto) akitolea ufafanuzi moja ya picha zilizopigwa mkoani Shinyanga wakati kukabidhi vyeti kwa wahitimu walionufaika na mafunzo mbalimbali kupitia mradi huo.
Subira akitoa ushuhuda kwa jinsi alivyopata ujauzito akiwa shuleni na alivyofanikiwa kutokana na Mradi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Japan.

Veronika Amosy akitoa ushuhuda na kueleza changamoto zilizomkuta mara baada ya kubeba mimba akiwa shuleni.

Mkufunzi Mkazi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Bw. Said Kayege kutoka mkoani Shinyanga akizungumza ni kwa namna gani wanavyotoa mafunzo hasa kwa mabinti waliopata mimba wakiwa mashuleni na kupelekea kuacha masomo yao.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu wa Wazima nchini, Dk. Fidelis Mafuniko akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa ripoti ya wazazi wenye umri mdogo walio pata mimba wakiwa shuleni.

Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues kwenye picha ya pamoja na wasichana waliopata mimba wakati wako masomoni ambao ni Veronika Amos (kushoto) pamoja na Subira (kulia).

Picha ya Pamoja

Na Mwandisi wetu

Shirika la Elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) lazindua Ripoti ya wazazi wenye umri mdogo walio pata mimba wakiwa shuleni, ambapo kama shirika waliweza kuwasaidia kwa kuwaanzishia mfumo maalumu utakao wasaidia katika kujiendeleza kielimu kwa kushirikiana na Elimu ya watu Wazima MOEVT. 

Akiongea wakati wa uzinduzi huo mgeni rasmi Kamishna wa Elimu kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufund (MOEVT)i nchini Prof, Eustella Bhalalusesa amesema cha kwanza ni kuishukuru serikali ya Tanzania kwa kuweka ushirikiano na shirika hili la UNESCO kwani ni jambo zuri hasa ukizingatia wote wanafanya kazi zinazo endana , cha pili nikuendelea kuungana kwa ajili ya kuweza kutoa elimu ya jinsia kwa ajili ya kuepuka mimba za utotoni kwa wanafunzi walioko mashuleni hivyo ameipongeza (UNESCO) kwa kutambua thamani ya watoto wa kike hasa wale walioshindwa kuendelea na masomo kwa kuwaanzishia njia mbadala za kuweza kuwafundisha kwa kuungana na elimu ya watu wazima kwani msingi wa watoto hao ni Elimu. 

Naye Mkuu wa Ofisi na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) nchini, Zulmira Rodrigues amesema wao kama shirika walianza kufanya mchakato wa kufanya tafiti kwa mikoa mbalimbali na kugundua kwamba watoto wengi wa jinsi ya kike wameweza kukatiza masomo yao kutokana na kupata mimba pindi wawapo shuleni ndipo walipoamua kuanzisha namna ya kuweza kumkomboa mtoto wa kike aweze kupata elimu inayoweza kumsaidia katika maisha yake kwa kuweza kuwasiliana na Mkurugenzi wa elimu ya watu wazima MOEVT na kuanzisha mchakato wa kuweza kuwakomboa kielimu.

Vilevile Bi. Rodrigues aliongeza kwa kusema wazazi waweze kukaa na watoto na kuwafundisha elimu ya kijinsia na kuweza kuwatatulia shida mbalimbali walizonazo kwani ndio hupelekea watoto kuingia katika tamaa mbalimbali hususani wakiwa katika hatua za mabadiliko ya mwili. 

Naye Balozi wa Japani nchini Tanzania Mh. Masaharu Yoshida amesema wazazi wenye umri mdogo Tanzania ni wengi na wanauhitaji wa kupata mafunzo ya Elimu kwa hali na mali hivyo kama ubalozi wa Japan umeamua kuanzisha mradi wa kuwasaidia wazazi hao mradi huo ambao unaratibiwa na (UNESCO) ulianza toka mwaka 2012 ambapo ulianzishwa na Bi.Zulmira Rodrigues, Mr. Min Jeong Kim na Jennifer Alima-Kotta uliogharimu kiasi dola za Kimarekani 400,653 kutoka Japanese Funds-in-Trust, Lengo kubwa ni kutaka kumkomboa mtoto wa kike ambaye amepata au alipata ujauzito akiwa shuleni, Pia alitoa shukrani kwa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) kwa kuweza kuwapa ushirikiano kuanzia walipoanza mpaka hivi leo na aliweza toa wito kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kwa kuomba kuendelea kupambana na mimba za wanafunzi wawapo mashuleni na kuendelea kutilia mkazo sheria zitakazo wabana watu wanao sababisha ujauzito kwa mtoto wa kike awapo shuleni. 

Aidha Ofisa Mipango ya Elimu wa Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Tanzania, Jennifer Kotta msimamizi wa mradi huo alieleza dhumuni la mradi na namna gani wameweza kufanikiwa pamoja na changamoto zake ambapo alianza kwa kueleza kuwa mradi huo sio rasmi ndio maana wameweza kushirikiana na elimu ya watu wazima kwani wanafunzi wengi wa kike huwa wanapata vishawishi mbalimbali pindi wawapo mashuleni na kuweza kuwa sababishia kuwa wazazi wadogo.

Kotta amesema kumekuwa na mambo mengi yanayo wakumba wanafunzi wa kike wawapo mashuleni na ndio husababisha madhara makubwa ambayo hupelekea wanafunzi hao kuwa wazazi wenye umri mdogo na bila kutegemea kwani ni ajabu na ni jambo la kusikitisha sana mtoto ana mlea mtoto mwenzake na kuwa na imani kuwa ndoto zake haziwezi timia kwa kutoendelea na masomo pindi awapo mjamzito au pindi akijifingua, ambapo aliwaomba wazazi kwani hali iliyopo kwa sasa kwa watoto wetu si nzuri sana tukumbuke kuwahimiza watoto kuhusu mila na desturi zetu na pia kuwa wafuatiliaji kwa nguvu zote kwani wazazi wengu huwa wanawadharau watoto wa kike kwa kudhani hawana msaada na ndipo yeye kama mtoto anaamua kuchukua uamuzi wake binafsi na kukuta wanaangukia katika hali ya kuwa mzazi mwenye umri mdogo vilevile aliweza kusisitiza kuhusu kuwalinda watoto wa kike hasa kipindi cha mabadiliko ya mwili ambapo ndipo changamoto mbalimbali hutokea kwa watoto hao hasa pindi wawapo mashuleni na hata mitaani. 


Hata hivyo mmoja ya wazazi wadogo walioweza kuchukuliwa na kusaidiwa na Shirika la (UNESCO) Tanzania, Chausiku Subira aliweza kutoa ushuhuda namna gani wanavyokumbana na changamoto hizo mpaka hatimaye kuwa wazazi katika umri mdogo wakiwa bado ni wanafunzi.

"katika safari yangu ya kimasomo mara baada ya kumaliza elimu ya msingi niliweza kuchaguliwa na kuendelea na elimu ya pili hapo ndipo ndoto zangu zilipoishia kwa kupata ujauzito ambao ulinipelekea kufukuzwa shule na hatimaye kurudishwa nyumbani jambo lililokuwa gumu kwangu kwani ujauzito huo ulikuwa sio wa kutegemea hasa ukizingatia mimi nikiwa bado mwanafunzi, nyumbani walinifukuza na kusababisha niwe na maisha magumu nisiyo ya tarajia nikizingatia nimepoteza shule pia hata ndugu hawanitaki lakini hiyo yote ni kutoka na na miundombinu ya shule tunazo soma kuwa mbali na makazi na kupelekea wanafunzi wengi kutembea kwa mguu umbali mrefu huku wakiwa na njaa na kuingia katika vishawishi mbalimbali", alisema Subira.

Pia Subira aliweza kutoa wito kwa serikali kwa kujenga mabweni katika shule mbalimbali na kuweza kuwatengenezea mazingira ya kuweza kurejea mashuleni pindi wanapojifungua kwa ajili ya kuweza kutimiza ndoto walizo kuwanazo pia kuweka sheria ambayo itakuwa inatenda haki kwa kila mmoja kwani imekuwa ni kwa mtoto wa kike tu kufukuzwa huku aliye sababisha ujauzito mtoto wa kiume kubaki akiendelea na masomo vilevile katika upande wa shule kuweza kutoa mafunzo kwa watoto wa kike kuhusu elimu ya jinsia na ninamnagani wanaweza wakajiepusha na vishawishi wanavyo kutananavyo.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)