Pages

UN, SERIKALI ZATAKA VIJANA KUONGOZA KATIKA KUKABILI MABADILIKO TABIA NCHI SINGIDA

IMG_4985
Mkuu wa wilaya ya Ikungi, Chigulu Charles akitoa neno la ukaribisho kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone katika ziara ya kukagua miradi inayofadhiliwa na Mashirika ya Umoja wa Mataifa mkoani Singida.

Na Modewjiblog team, Singida
MRATIBU wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi mkazi wa Shirika la Mipango ya Maendeleola umoja huo (UNDP) Bw.Alvaro Rodriguez, amezuru mradi wa ufugaji nyuki uliopo Ikungi mkoani Singida.
Katika Ziara hiyo kwenye mradi unaofadhiliwa na UNDP, Mratibu huyo aliambatana na Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone, na Ofisa wa Mambo ya Nje kutoka Kitengo cha Ushirikiano wa Kimataifa wizara ya Mambo ya Nchi za Nje, Bi. Maulidah Hassan.

Viongozi hao walifika katika mradi huo kuangalia mafanikio ya mradi huo unaotekelezwa chini ya mpango wa miaka mitano wa Msaada wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa, (UNDAP).

Mradi huo uliofadhiliwa na UNDP kwa thamani ya Shilingi milioni 224 umewanufaisha wafugaji 2,000 huku wanawake wakiwa ni 1,100.
Mradi huo ulianza kutekelezwa kuanzia mwaka 2013 na 2014 umelenga kuendeleza shughuli za ufugaji nyuki wilayani Ikungi.

Aidha mradi huo umelenga kupunguza umaskini kutunza mazingira kwa njia ya uragibishi na kufunza wananchi kuhusu suala la ufugaji nyuki na utunzaji wa mazingira.

Kutokana na mradi huo, fursa za ajira zilitengenezwa, hasa vijana wa kijijini, kuwepo na eneo la kisasa la kutengeneza mizinga ya nyuki na uchomaji moto uliokuwa unafanywa katika misitu ukapungua sana.
Akizungumza katika eneo la mradi Bw. Rodriguez, aliusifu utawala wa mkoa wa Singida kwa kufanyakazi na UNDP kwa lengo la kujenga uwezo kwa wananchi na wakati huo huo kutunza mazingira.
IMG_4998
Mwakilishi wa Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi, inayosimamia mradi wa ufugaji nyuki kisasa, Boniface Mathew akitoa maelezo ya mradi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez. Pamoja na mambo mengine Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP limeshiriki katika ufadhili wa utengenezaji wa mizinga bora pamoja na kutoa semina mbalimbali kwa wafugaji nyuki uliogharimu kiasi cha Shilingi milioni 224 hadi sasa.

“Ninafuraha sana kuona matokeo mema ya mradi huu; ni lengo letu kutunza mazingira huku tukifaidika na uhifadhi huo. Mafanikio haya yanastahili kuigwa na wengine,” alisema Rodriguez akiongeza kuwa wanawake walifaidika sana na mradi huu kiasi cha kustahili kufanyiwa kazi katika eneo jingine.

Mkuu wa mkoa wa Singida Dk. Parseko Kone alisema mradi wa UNDP una matokeo yenye tija kubwa na kuwataka waliofadhiliwa kutumika kufunza jamii nyingine umuhimu wa ufugaji na hifadhi ya misitu.
“leo tunashuhudia ufugaji nyuki wa kisasa ambao umebadilisha sekta ya ufugaji nyuki, tija katika ufugaji huu imeongezeka maradufu. Hiyo imesaidia kaya zaidi ya 1000 kupata kipato cha kukabiliana na umaskini.” Alisema Mkuu wa mkoa.
Aidha alisema kwamba wafugaji nyuki wameweza kuwa pamoja na kujipatia asali na mazao mengine kutokana na shughuli ya ufugaji nyuki kama nta, sumu ya nyuki, uchavuaji na kadhalika.
IMG_5016
Mwakilishi wa Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi, Boniface Mathew (kulia) akikabidhi taarifa ya mradi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Kutokana na shughuli hizo za ufugaji zaidi ya fursa 2,500 za ajira zilitengenezwa.nafasi hizo ni kama za mfugaji, wachongaji mizinga, wauza asali, wasafirishaji na wachakati wa asali.
Wilaya ya Ikungi imejaliwa kuwa na misitu ya Miombo na Minanga ambayo ni chanzo kizuri cha chavua.
Mradi wa ufugaji nyuki Ikungi umelenga kufungua njia zote za uzalishaji asali na kupiga vita umaskini kwa kuanzisha fursa za ajira za kujitegemea.
Mwakilishi huyo wa UNDP na Mkuu wa mkoa pia walitembelea hospitali ya rufaa ya mkoa ambayo ipo katika awamu ya mwisho ya ujenzi.
Itakuwa ni moja ya hospitali kubwa itakayohudumia mikoa mitano katika ukanda wa kati.
Katika mazungumzo yake Mratibu wa UN alimpongeza Mkuu wa mkoa kwa juhudi zake za kuhudumia wanawake waume na watoto wa Tanzania.
IMG_5009
Baadhi ya mizinga ya kisasa iliyofadhiliwa na UNDP ikiwa kwenye karakana ya kutengeneza mizinga ya nyuki tayari kugawiwa kwa vikundi mbalimbali vya wanawake na vijana iliyopo kwenye Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi.
IMG_5022
Mwakilishi wa Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi, Boniface Mathew akimwonyesha mizinga ya kisasa ya ufugaji nyuki Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (katikati). Kushoto ni “Programme Assistant- Global Environmental Facility Small Grant”, UNDP, Stella Zaa.
IMG_5077
Malengo ya maendeleo endelevu sasa yamewafikia wafugaji wa nyuki Singida na waratibu wa miradi ya wafugaji wa nyuki Singida. Pichani ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez katika karakana ya kutengenezea mizinga ya kisasa.
IMG_5086
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na wanakikundi cha Uaminifu kinachojihusisha na ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa mara baada ya kuwasili kukagua shamba darasa la kuzalisha makundi ya nyuki lilipo katika kijiji cha Mahambe tarafa ya Ikungi mkoani Singida.
IMG_5098
Mwakilishi wa Mratibu Mkuu wa Taasisi ya Kijamii ya Fursa za Kimaendeleo (Fu-DI) ya wilayani Ikungi, Boniface Mathew akijiandaa kumvisha nguo maalum Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone kabla ya kuingia kwenye shamba darasa la kuzalisha makundi ya nyuki lilipo katika kijiji cha Mahambe tarafa ya Ikungi mkoani Singida.
IMG_5101
Mwanakikundi cha Uaminifu kinachojihusisha na ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa, Juma Simbu, akitoa taarifa ya kikundi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone ambapo alisema mradi wa ufugaji utawatoa kwenye lindi la umaskini, japokuwa wanakabiliwa na changamoto kadhaa.
IMG_5102
Mwanakikundi cha Uaminifu kinachojihusisha na ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa, Juma Simbu akikabidhi taarifa ya kikundi kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_5109
Sehemu ya eneo la shamba darasa la kuzalisha makundi ya nyuki lilipo katika kijiji cha Mahambe tarafa ya Ikungi mkoani Singida.
IMG_5114
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisaidiana na wanakikundi cha Uaminifu kinachojihusisha na ufugaji nyuki kwa njia ya kisasa kupandisha moja kati ya mizinga iliyofadhiliwa na UNDP katika shamba darasa la kuzalisha makundi ya nyuki lilipo katika kijiji cha Mahambe tarafa ya Ikungi mkoani Singida.
IMG_5123
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Singida, Dkt. Parseko Kone wakipandisha moja kati ya mizinga iliyofadhiliwa na UNDP kwenye shamba hilo.Kwa matukio zaidi bofya hapa

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)