Pages

Sir Alex: Itakuwa ujinga kumfuta Mourinho


Image captionSir Alex: Itakuwaujinga kumfuta Mourinho
Aliyekuwa mkufunzi wa Manchester United,Sir Alex Ferguson ,amesema ''itakuwa ujinga'' mmiliki wa Chelsea Roman Abrahimovich kumfuta kazi Jose Mourinho
Mabingwa hao watetezi wamesalia katika nafasi ya 14 baada ya kupoteza mechi 8 kati ya 15 za kwanza msimu huu.
Duku duku zinasema kuwa kibarua cha kocha huyo mbishi huenda kikaota nyasi endapo the Blues watashindwa tena katika mechi zao 2 zijazo.
Hata hivyo kocha mwenza Ferguson amemtetea akisema hakuna haja ya kumtimua kocha huyo mwenye tajriba kuu kufuatia msimu huu mbaya.
Ferguson badala yake anapendekeza Abrahimovich avumilie kidogo upepo huu mbaya ukipita kocha Mourinho atairejesha timu hiyo katika mahala inakostahili.
''hakuna haja ya kufuta mmoja wa wakufunzi hodari kama Jose''
''Tayari amewafuta kazi watu wengi sana katika kipindi cha miaka 10 tu tangu ainunue klabu hiyo ya Stamford Bridge''
"nafkiri kufikia sasa ameshajua kuwa haifai hivyo.''
Image copyrightPA
Image caption''Sharti awe na imani, Mourinho ameshinda vikombe vikubwa kila taifa alikoenda, itakuwa ni ujinga kumfuta kazi.'' Ferguson
''Sharti awe na imani, Mourinho ameshinda vikombe vikubwa kila taifa alikoenda, itakuwa ni ujinga kumfuta kazi.''
'Hiyo bila shaka ni usimamizi duni.'
Mourinho alirejea Chelsea mwaka wa 2013 na akatwaa kombe la Capital One.
Taji hilo linaongezea kwa yale ya , FA mbali na mataji mawili ya ligi kuu ya Uingereza alizoshinda mwaka wa 2004 na 2007.
Alipotoka Stamford Bridge alishinda mataji mawili akiwa na Inter Milan na mawili akiwa kocha wa vigogo wa ligi ya Uhispania Real Madrid.
"Hii ndio mara ya kwanza kwake kukosa ushindi wa aina yeyote tangu awe kocha alisema Ferguson katika hadhara ya TechCrunch Disrupt London .
''bila shaka atapata suluhu ya mkwamo huu Stamford Bridge.''
Jumamosi ijayo Chelsea itachuana na vinara wa ligi hiyo Leicester, chini ya kocha wao mpya Claudio Ranieri
Leicester wana alama 17 zaidi ya Chelsea.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)