Pages

Neno la Kuaga Mwaka 2015 na Kuukaribisha Mwaka 2016. Asanteni Wadau

Yakiwa yamebaki masaa machache kuumaliza mwaka 2015 na kuukaribisha mwaka mpya 2016 kwanza napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi kwa neema na rehema zake kunifikisha hapa nilipo leo nikiwa mzima wa afya na mwenye tumaini mbele zake.

Pia nachukua nafasi hii kumshukuru Mungu wetu na baba yetu kwa mambo mengi aliyotutendea na anayoendelea kututendea hakika si kwa uwezo wetu bali ni kwa neema na rehema zake.
Namshukuru pia kwa kuweza kunisimamia na kunipitisha kwenye majaribu ambayo kiukweli peke yangu siyawezi lakini kwa msaada na uwepo wake amenisaidia kuyavuka na kuyashinda mengi.

Tukikaribia kumaliza mwaka 2015 napenda kuwashukuru kwanza Wazazi wangu kwa ushirikiano wao wote tokea mwaka huu unaanza hadi leo tunapokaribia kuumaliza mwaka, vilevile niwashukuru sana Dada zangu, kaka zangu kwa mazuri yao yote waliyonitendea hakika bwana wetu na Mungu wetu atawaongezea maradufu pale mlipotoa. Nachukua nafasi hii kuwashukuru marafiki zangu wa facebook, mtaani, ofisini na popote pale kwa ushirikiano wenu mlionipa tokea mwanzo wa mwaka 2015 hadi leo tunaenda kuumaliza mwaka nawashukuru sana na mwenyezi Mungu awatie nguvu, baraka na neema zake zipate kuwatembelea.

Nawashukuru pia wadau wote wa Lukaza blog ambao wameweza kufanya kazi na sisi kuhakikisha lukaza blog inaendelea kung'ara ndani na nje ya nchi na kuifanya Lukaza blog kufanikiwa kuibuka na Tunzo ya Blog Bora katika Kipengele cha Siasa katika shindano la African Blogger Awards 2015 lililofanyika Afrika Kusini na lukaza blog kuwa mmoja wa washindi katika kipengele kimoja wapo na kuufanya mwaka 2015 kuwa mwaka wa mafanikio kwa Timu nzima ya Lukaza Blog ukiwemo na wewe msomaji wetu na mdau wetu.Tunajipanga kuendelea kuwaletea mazuri zaidi kwa mwaka 2016.

Mwaka 2015 ulikua mwaka mgumu sana kwangu kutokana na kupitia majaribu ambayo kwangu ni mazito sana na peke yangu siwezi kuyavuka lakini naamini Kwa uwepo wake Rahabanah naamini leo ataenda kutenda miujiza yake na kufanikisha kunivusha kwenye hili jaribu Kama ambavyo kila jaribu huwa na mlango wa kutokea na Mungu wetu hampi mja wake jaribu linalomzidi kimo au uwezo basi naamini jaribu hili naenda kulimaliza leo mbele za bwana.Kikubwa ni kuwa na imani mbele zake huku tukiwa wanyenyekevu mbele zake.

Napenda kuchukua nafasi hii kuwasamehe wale wote walionikosea either kwa makusudi au bila hata kujua ili na mimi mnisamehe wote niliowakosea kwa makusudi kabisa na hata wale niliowakosea bila hata kujua kwa maana msamaha wenu kwangu ndio na mimi nitaweza kusamehewa mbele ya Mungu wetu kwa kipimo kilekile ili kuweza kuingia mwaka 2016 tukiwa na mioyo safi isiyokuwa na hata chembe za hasira, masimango, chuki na uhasama.

Nachukua nafasi hii Kuendelea kuwashukuru wote na kuwasihi kuendelea na umoja, ushirikiano na kupendana

Nachukua nafasi hii kuwatakia watanzania wote na dunia nzima heri ya Mwaka mpya 2016.

Josephat Lukaza
Founder /Chief Editor
Lukaza Blog
http://www.josephatlukaza.com

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)