Pages

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde afanya ziara makao makuu ya Tigo

Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  akizungumza na wafanyakazi wa tigo baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijtonyama  jijini Dar es laam 
Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akizungumza na waandishi wa habari na wafanyakazi wa tigo   baada ya kufanya ziara mapema leo  katika makao  makuu ya Tigo kijitonyama Dar es laam 


Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez , akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) katika mkutano alioshiriki pia Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde  baada ya kufanya ziara katika makao  makuu ya Tigo Kijtonyama  jijini Dar es laam
Dar es Salaam, 30th December 2015- Tigo Tanzania leo imepokea kwa furaha ugeni wa ghafla wa Naibu waziri wa Wizara ya Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Antony Mavunde alipotembelea makao makuu ya kampuni hiyo yaliyoko Kijitonyana jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mavunde ambaye alikuwa ameongozana na waandishi wa habari na maofisa kutoka ofisi za uhamiaji alitinga ofisini hapo mnamo saa nne asubuhi ya Jumatano ya tarehe 30 Desemba na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Tigo, Bwana Diego Gutierrez pamoja na wafanyakazi wengine wa kampuni ya Tigo.
Bwana Gutierrez alimtembeza Naibu Waziri kwenye idara mbalimbali za kampuni hiyo huku akitambulisha huduma zinazotolewa na kujibu maswali yaliyokuwa yakiulizwa na Mhe. Waziri.
Kampuni ya Tigo imekuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya mawasiliano kwa kutoa huduma na bidhaa zenye ubunifu na manufaa makubwa kwa jamii, hivyo kuchangia kwa kiasi kukubwa sana kuendeleza sekta hii muhimu kupitia njia mbali mbali kama kutoa ajira, kuchangia pato la taifa, kuchangia maendeleo ya jamii na kuwezesha watanzania wajiendeleze kiuchumi na kijamii kupitia mawasiliano ya bei nafuu.

Bwana Gutierrez alisema kampuni ya Tigo imefurahishwa mno na ugeni huo huku akiongeza kuwa ugeni huo unadhihirisha kwamba serikali imeonesha kwamba inajali huduma zinazotolewa na mashirika ya sekta binafsi.
Bwana Gutierrez alisema “Tutaendelea kushirikianana na serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kuwa sekta ya mawasiliano inakua zaidi na inaleta mabadiliko lukuki kwenye maisha ya watanzania na nchi nzima kwa ujumla. Tigo imejikita kwenye kupanua wigo wa mawasiliano kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anaweza kuwasiliana kwa bei nafuu, kupitia mtandao bora na wenye huduma zenye uhakika".

Kuhusu kuitembelea Tigo, Mh. Mavunde alisema: "leo tumetembelea kampuni ya Tigo, kwa ajili ya kujitosheleza vipi kampuni hii inajali waajiri wake, na katika ziara hii tumebaini mambo kadha ambayo tungependa kampuni ya Tigo, ivifanyie kazi kwa mfano kwenye maswala ya afya na usalama, na pia tungependa kuona mikataba baina ya Tigo na watoa huduma wake, pia serikali ya awamu ya tano, ipo makini kuhakikisha sheria inafuatwa ili tuwe na jamii inayozingatia sheria"

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)