Pages

Makamu wa Rais mgeni rasmi Tamasha la Amani

msa1
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kinondoni wakati alipomtangaza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Mh. Samia Hassan Suluhu kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Kushukuru kufuatia kufanyika kwa uchaguzi wa amani na utulivu tarehe 25 mwezi Oktoba mwaka huu nchini kote huku nchi ikiendelea kuwa na utulivu na amani ya hali ya juu. Kushoto ni Mratibu Tamasja la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe
msa2
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na Mratibu Tamasja la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe wakifurahia jambo wakati walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari leo.
msa3
Mratibu Tamasha la Kushukuru masuala ya usalama Bw. Hamisi Pembe akifafanua mambo mbalimbali kuhusu usalama wa tamasha hilo, huku Mkurugenzi wa Msama Promotion akimsikiliza kwa makini wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari
............................................................................
NA MWANDISHI WETU
·Munishi aliyeimba Malebo naye ndani
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Samia Suluhu Hassan amethibitisha kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Krismass litakalofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Mwewnyekiti wa kamati ya maandalizi ya kamati hiyo Alex Msama amesema kuwa Makamu wa Rais amethibitisha na wanaendelea kujipanga ili kulinogesha Tamasha hilo.

Alisema wanashukuru kwa Makamu wa Rais kushiriki katika Tamasha hilo kama mgeni rasmi licha ya muda mfupi tangu aingie madarakani. Msama alisema, mama Samia ameonyesha kuwa ni mzalendo wa kweli kwani muda sio mrefu amemaliza kampeni za Uchaguzi Mkuu na kuzunguka nchi nzima hivyo kuwa na uchovu mwingi lakini amekubali kitu ambacho kimetoa faraja kwa wakazi wa Dar es salaam ambao wanatarajia kumiminika kwa wingi kushiriki tamasha hilo.

“Napenda kuwatangazia kuwa mgeni rasmi wa Tamasha la Krismass lenye lengo maalum la kushukuru mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu kuwa mgeni rasmi ni mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan,” alisema Msama. Msama amesema kutokana na Makamu wa Rais kuwa mwanamke wa kwanzakushika nafasi hiyo hapa nchini kuna kila sababu ya mashabiki kujitokeza kwa wingi siku hiyo.

Katika hatua nyingine Msama pia amemtangaza mwimbaji wa injili mkongwe hapa nchini anayefanya shughuli zake nchini Kenya Faustine Munishi ambaye ameimba nyimbo maarufu inayojulikana kama Malebo.

Amesema Munishi amethibitisha na yuko katika mazoezi ya nguvu kuhakikisha kuwa kila kitu kinakwenda sawa siku hivyo na amepanga kuimba nyimbo zote ambazo alikuwa akiimba zamani ikiwemo malebo.

Aidha mjumbe wa kamati ya Tamasha hilo Khamis Pembe alisema, kila kitu kimekamilika ili kuhakikisha washiriki akiwemo Makamu wa Rais wanakuwa salama.
Alisema wamejipanga vizuri na watahakikisha hakuna tatizo lolote la ulinzi siku hiyo ili kuendeleza hali hiyo kama ilivyokuwa katika matamasha mengi ambayo yamekuwa yakiandaliwa na Msama Promotions.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)