Pages

ENKI YA BARCLAYS TANZANIA YAZINDUA KAMPENI YA KADI ZAKE ZA VISA KWA AJILI YA WATEJA

 Meneja wa Bidhaa wa Benki ya Barclays Tanzania, Valence Luteganya (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa uzinduzi wa kampeni ya kadi zake za Visa kwa ajili ya kuwarahisishia wateja wao. Kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa benki hiyo, Joe Bendera.
 Wapiga picha wakichukua picha meza kuu wakati wa uzinduzi huo.
 Meneja wa Bidhaa wa Benki ya Barclays Tanzania, Valence Luteganya (wa pili kulia), akisisitiza jambo katika mkutano huo. Kutoka kulia ni Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa benki hiyo, Joe Bendera, Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa benki hiyo, Oscar Mwamfwagasi na Meneja Bidhaa, Erica Mwaipopo.
 Mkuu wa Kitengo cha Bidhaa wa benki hiyo, Oscar Mwamfwagasi (kushoto), akitoa ufafanuzi wa matumizi ya kadi hiyo kwa waandishi.
Maofisa wa benki hiyo wakionesha kadi hiyo baada ya kuzinduliwa. Kutoka kulia ni Mkuu
wa Idara ya Mawasiliano na Masoko wa benki hiyo, Joe Bendera, Meneja wa bidhaa wa benki hiyo, Valence Luteganya, Mkuu wa
Kitengo cha Bidhaa wa benki hiyo, Oscar Mwamfwagasi na Meneja Bidhaa,
Erica Mwaipopo.

Na Dotto Mwaibale

BENKI ya Barclays Tanzania imezindua kampeni ya kadi zake za Visa kwa ajili ya kuwarahisishia wateja kupata huduma mbalimbali katika hali ya usalama wa fedha zao.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, Meneja wa Bidhaa wa benki hiyo, Valence Luteganya alisema wanayofuraha kwa kuzindua kampeni hiyo ambayo ni muhimu kwa wateja.

"Kampeni hii itafanyika kwa muda wa miezi mitatu kuanzia Desemba 15, 2015 hadi Februari 28, 2016 " alisema Luteganya.

Alisema kwamba kampeni hiyo itawawezesha wateja kunufaika na mafao mbalimbali yanyohusiana na malipo ya kabla na baada ya kutumia kadi zao za visa.

Alisema wateja wataweza kula na kunywa na kulala kwa punguzo la bei kwenye baadhi ya hoteli mbalimbali zilizopo jijini Dar es Salaam na kuwa punguzo hilo ni kwa ajili ya wateja wote wa Benki hiyo wanaotumia kadi zao za Visa popote walipo.

Luteganya alisema mafao hayo yatahusisha punguzo kutoka Hoteli ya Souththern Sun na Double Tree by Hilton na kuwa wateja  wataweza kulipia huduma mbalimbali kwa kutumia kadi hizo katika maduka ya ndani na nje ya nchi kama kulipia bidhaa za vyakula na matumizi ya nyumbani pamoja na kulipia kutumia mitandao.

Alitaja huduma zingine ambazo mteja anaweza kulipia ni kulipia huduma za simu za mkononi, kutoa pesa katika ATM nje na ndani ya nchi na kulipia mafuta ya gari katika vituo vya Engen cha Mikocheni jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)