Pages

WAFANYAKAZI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAFANYA BONANZA LA KUMUAGA MAKAMU WA RAIS MSTAAFU

 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Kombe Nahodha wa timu ya VPO
Sports Club, Nehemia Mandia, baada ya kuibuka na ushindi katika Bonanza maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4.
  Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Cheti cha kushiriki Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, katika Bonanza
maalum la kumuaga Dkt. Bilal, lililofanyika jana Nov 28, 2015 kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam. VPO waliibuka kidedea baada ya kuwafunga timu ya Wizara ya Mambo ya Nje kwa mikwaju ya penati 5-4.
  Katibu Mkuu wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Sazi Salula, akizungumza wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt.
Mohammed Gharib Bilal, liliandaliwa na timu ya timu ya Ofisi ya Makamu wa Rais (V.P.O Sports Club) lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete, uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam jana Nov 28, 205. Katika Bonanza hilo lililoshirikisha jumla ya timu Nne za VPO Sports Club, Wizara ya Mambo ya Nje, Kamati ya Amani waliochanganyika na Mabalozi na Amana Bank waliochanganyika na Zanzibar Fc, Timu ya VPO Sports Club iliibuka na ushindi kwa kuwafunga Mambo ya nje kwa jumla ya mikwaju ya penati 5-4 na kutwaa kombe la Bonanza hilo
 Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamuuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wanamichezo baada ya kumalizika Bonanza la kumuaga, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana

 Nahodha wa timu ya VPO Sports Club, Muhidin Sufiani, akimtoka beki wa timu ya Kamati ya Amani, Mhungaji Amos Nene, wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo  kumalizika bila kufungana
  Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani Tanzania, Sheikh Alhad Mussa Salum, akimiliki mpira mbele ya beko wa VPO Sports Club,Bakari Kibiti wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo  kumalizika bila kufungana.
 Mchezaji wa  VPO Sports Club, Nehemia Mandia, akimtoka beki wa timu ya Kamati ya Amani, Mhungaji Amos Nene, wakati wa Bonanza maalum la kumuaga Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, lililofanyika kwenye Uwanja wa Jakaya Kikwete,uliopo Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam  jana Nov 28, 2015. Katika Mchezo huo VPO walishinda kwa bao 1-0 na kutinga fainali na Timu ya Mambo ya Nje ambapo pia waliibuka kidedea kwa mikwaju ya penati 5-4 baada ya mchezo  kumalizika bila kufungana

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)