Pages

WATANZANIA WATAKIWA KULINDA SHAHADA ZAO ZA KUPIGIA KURA

 Wakazi wa mji wa Singiga na vitongoji vyake wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akijinadi na kuwaomba wampigie kura za ndio ifikapo Oktoba 25 Mwaka huu kwenye uchaguzi mkuu wa Urais,Wabunge na Madiwani.
 Harakati za kusaka nafasi ya juu  ya uongozi katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo zimepiga kambi mkoani Singida kwa mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi CCM, Dkt John Pombe Magufuli pichani kuwahutubia maelfu ya wananchi waliokusanyika katika uwanja wa Pipoz mjini humo kwenye mkutano wa kampeni.

Dkt Magufuli ameishauri tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC kutimiza wajibu wake wa kutenda haki kwa wagombea wote wa ngazi za Uraisi,pia amewataka Wananchi wakatae kulaghaiwa na baadhi ya watu wanaotaka madaraka kwa nguvu,kwa kuzinunua shahada zao za kupigia kura,badala yake amewaomba wazitunze shahada hizo ili ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wapige kura. PICHA NA MICHUZI JR-SINGIDA
 Maelfu ya Wananchi wa Singida wakimshangilia Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia na kujinadi kwa kuwaomba ridhaa ya kuwaongoza iwapo watamchagua kuwa Rais ifikapo Oktoba 25 mwaka huu,kwenye uchaguzi mkuu,Dkt Magufuli amewaomba wananchi hao alipokuwa akiwahutubia kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya Pipoz,mjini Singida.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi,Dkt Joh Pombe Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Singida mjini Mussa Sima mbele ya maelfu ya Wananchi (hawapo pichani) kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Pipoz mjini Singida jioni ya leo.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimnadi mgombea Ubunge jimbo la Iramba Magharibi kwa wakazi wa Iramba mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara,mara baada ya kumkabidhi Ilani ya chama hicho.

 Wananchi
wakiwa wamefunga barabara wakizuia msafara wa Mgombea Urais Dkt John
Pombe Magufuli katika kijiji cha sepuka na Ndago,wakati msafara huo
ukielekea Iramba kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Dkt
John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mwigulu Nchema kabla ya
mkutano wa hadhara wa kampeni kuanza mjini Kiomboi,wilayani Iramba.
 Mgombea
Ubunge wa jimbo la Iramba Magharibi,Mwigulu Nchemba akiwahutubia
wananchi wa Kiomboi mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni.
Baadhi
ya Kadi za Wanachama wa Chadema zilizokabidhiwa kwa Mgombea Urais wa
CCM Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa shule
ya msingi Kiomboi,Wilayani Iramba mapema leo mchana.
Msafara
wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli ukikatiza katika bonde
la mto Sibiti kupitia barabara ya Nduguti kuelekea wilayani
Mkalama,kwenye mkutano wa kampeni mapema leo mchana.
 
Ujenzi wa Daraja la Sibiti wilayani Mkalama likiwa katika hatua za
mwisho kukamilika,Daraja hilo limeleta matumaini mapya kwa wakazi hao wa
Mkalama,kwani wakati wa mvua ilikuwa ni kikwazo kikubwa kwao wakati wa
kusafiri na hata kusafirisha mazao yao ya biashara.
 Wakazi wa kijji cha Mtinko wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,aliposimama na kuwasalimia.
Wakazi
wa kijiji cha Mtinko wakiwa wamefunga barabara wakitaka Mgombea Urais
wa CCM Dkt Magufuli awasikilize shida zao ili akiingia madarakani aweze
kuwasaidia
 Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji cha
Ilongero,Singida Vijijini mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni.
 Wananchi
wa Singida na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika kwenye uwanja wa
People's,mjini Singida katika mkutano wa kampeni wakimsikiliza Mgombea
Urais wa CCM Dkt Magufuli kabla ya kuanza kuwahutubia jioni ya leo.
 
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu Mwigulu Nchemba akiwaomba wakazi
wa mji wa Singida na vitogoji vyake waliofurika kwenye mkutano wa
kampeni,kuwa ifikapo Oktoba 25 mwaka huu wajitokeza kwa wingi kumpigia
kura za ndio za kutosha Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli pamoja na
Mbunge na Madiwani ili wapate ushindi wa kishindo. 


Mjumbe wa Kamati ya Kampeni CCM,Ndugu January Makamba akimuombea kura
za kutosha mmgomea Urais wa CCM Dkt Maguli pamoja na Mbunge na Madiwani
wa Singida mjini kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa
Pipoz mjini humo.
Baadhi
ya Kadi za Wanachama wa Chadema zilizokabidhiwa kwa Mgombea Urais wa
CCM Dkt Magufuli,kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa shule
ya msingi Kiomboi,Wilayani Iramba mapema leo mchana.
 Maelfu
ya wakazi wa Singida wakiwa kwenye mkutano wa kampeni za Urais wa CCM
Dkt John Pombe Magufuli,uliofanyika katika uwanja wa Pipoz mjini humo.
Aliyekuwa
Mbunge wa Singida Mjini (Mbunge Mstaafu),Mohamed Dewji akimwombea kura
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli kwa wananchi wa Singida na
vitongoji vyake katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa
Pipoz,mjini Singida,Dewji pia ametangaza kumuunga mkono aliyemrithi kiti
chake cha Ubunge,Ndugu Mussa Sima.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)