Pages

Watanzania washauriwa kuzingatia Afya bora ya Moyo


Watanzania washauriwa kuzingatia Afya bora ya Moyo
Dar Es Salaam, Oktoba 2015: Ikiwa zimepita siku tatu toka kuhadhimishwa siku ya Moyo duniani mwaka huu, Watanzania wameshauriwa kufanya maamuzi binafsi katika kujali afya ya moyo. Kauli mbiu ya Siku ya Moyo duniani mwaka 2015 inahusu kuchagua afya bora ya moyo kwa kila mtu na kila mahali. Pia inalenga kuonyesha matokeo ambayo mazingira yetu yanaweza kuleta juu ya uwezo wetu wa kufanya maamuzi bora kwa ajili afya bora kwa moyo wa binaadamu. Pia siku hiyo inatumika kuelimisha jinsi ambavyo mazingira tunayoishi yanaweza kuathiri na kuongeza hatari ya magonjwa yanayohusiana na moyo.

Kwa mujibu wa takwimu ya hivi karibuni ya WHO iliyochapishwa Mei 2014, vifo vya ugonjwa wa moyo nchini Tanzania vimefikia 11,031. Hii ni sawa na wastani wa vifo 54 kwa kila watu 100,000, na hivyo kuiweka Tanzania nchi ya 148 duniani. Idadi hii ya vifo inayosababishwa na matatizo ya moyo inahitaji mabadiliko haraka sana ikibidi kusitishwa kabisa.
Ikiwa chanzo kikubwa cha vifo vingi duniani, magonjwa ya moyo yakiwa ni pamoja na ugonjwa wa mshtuko wa moyo, ugonjwa wa mishipa ya mfumo wa fahamu (kiharusi), shinikizo la damu, ugonjwa wa mishipa ya ateri, ugonjwa wa moyo kupooza, ugonjwa wa moyo wa kurithi na moyo kushindwa kufanya kazi yanaigharimu nchi kiuchumi na kijamii kwa kiasi kikubwa. Watanzania wengi wanakufa kwa magonjwa yanayohusiana na moyo kila mwaka, hali ambayo inahitaji hatua madhubuti na msaada wa kimkakati wa wadau wa maendeleo ili kubadili hili. Mambo hatarishi ya kitabia na ya kisaikolojia yanadaiwa kuchangia 75% ya magonjwa ya moyo. Kwa kweli, magonjwa mengi yanayohusiana na moyo yanaweza kuzuiwa kwa kushughulikia mambo hatarishi.

Dkt. Manoj Kumar Agarwala, Mshauri Mwandamizi na Mtaalamu wa Magonjwa ya Moyo na Mishipa ya Moyo katika Hospitali ya Apollo Hyderabad, anataja baadhi ya mambo hatarishi yanayoweza kusababisha ugonjwa wa moyo. Mambo hayo ni pamoja na umri, jinsia, historia ya familia, sigara, lishe duni, shinikizo la damu, kiwango kikubwa cha mafuta kwenye damu, kisukari, unene wa kupindukia, kutofanya mazoezi, dhiki na hali duni ya usafi. Dkt. Agarwala anapendekeza kuacha kuvuta sigara, kupunguza mafuta, kudhibiti shinikizo la damu, kuwa mchangamfu, kula mlo kamili, kuzingatia uzito unaotakiwa kama njia bora ya kupunguza hatari za magonjwa ya moyo na mishipa. Anaongeza kuwa mazingira ambayo tunaishi, kufanya kazi na kushiriki michezo yanaweza kuwa na matokeo makubwa juu ya  uwezo wetu wa kufanya maamuzi sahihi kwa afya ya mioyo yetu. 

Maisha ya shughuli nyingi pamoja na uhaba wa mlo kamili, matumizi ya tumbaku, ukosefu wa mazoezi vinaongeza kiwango cha vifo vinavyotokana na moyo nchini Tanzania. Mabadiliko katika maisha yanahitaji mchanganyiko wa hatua binafsi na hatua za kijamii na kiuchumi vilevile.
Tunaamini kwamba kila mtu, kila mahali ana haki ya kuchagua kuimarisha afya bora ya moyo. Kujenga mazingira ya afya ya moyo yatatuwezesha sote kufanya maamuzi sahihi yanayoweza kupunguza hatari ya ugonjwa wa moyo na kiharusi. Anathibitisha Mtaalamu huyo wa moyo kutoka Hospitali ya Apollo.

Kama moja ya sababu muhimu za afya ya moyo, Dkt. Girish B Navasundi Mshauri Mwandamizi, Mtaalamu magonjwa ya Moyo katika Hospitali ya Apollo, Bangalore, anawaelimisha Watanzania juu ya umuhimu wa maji ya kunywa ili kuepuka magonjwa ya moyo, utamaduni ambao Watanzania wengi hawana. "Moyo hauwezi kupiga bila maji, asilimia 70 ya mwili wa binadamu ni maji. Kwa hiyo, kufikia homiostasisi ya maji na elektroliti ni muhimu kwa ajili ya utendaji mzuri wa mwili, hasa mfumo wa mishipa ya damu. Anasema.

"Mwili Binadamu unahitaji karibu 35 ml za maji kwa kilo ya uzito wa mwili kwa siku hiyo ni karibu 2,100 ml kwa kilo 60 mtu. Matumizi ya glasi tano au zaidi za maji kwa siku kwa kiasi kikubwa hupunguza matukio ya janga la mashambulizi ya moyo, ikilinganishwa na kushindwa kunywa chini ya glasi mbili za maji kwa siku. "Anaongeza Dkt. Navasundi.

Dkt. Navasundi anahitimisha kwa kusema faida za matumizi ya kutosha ya maji hufanya damu kuwa nyepesi, kufanya mzunguko wake kwenda vizuri katika mfumo wa moyo, itapungua kazi kubwa ya moyo na hupunguza hatari ya damu kuganda papo kwa papo ndani ya mishipa ya damu.

Siku ya moyo inalenga kuboresha afya duniani na kuhimiza watu kufanya mabadiliko ya mtindo wa maisha na kukuza elimu kimataifa kuhusu njia za kuweka moyo wako na afya njema. Siku ya Moyo Dunia mwaka huu, imelenga katika kujenga chaguo sahihi la afya ya moyo kwa kila mtu, kila mahali kwa kuhakikisha kuwa watu wana uwezo wa kufanya maamuzi juu ya afya ya moyo popote pale wanapoishi, kufanya kazi na kushiriki michezo. Siku hii inatuhimiza sote ili kupunguza hatari za moyo na mishipa, na kukuza sayari yenye afya ya moyo kwa wale walio karibu nasi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)