Pages

TAASISI YA WANAWAKE WAHASIBU TANZANIA KUZINDULIWA HOTELI YA HYATT REGENCY

 Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake Wahasibu Tanzania (TAWCA), Neema Kiure- Mssusa (wa pili kulia), akiwaonesha waandishi wa habari cheti cha usajili wa taasisi hiyo Dar es Salaam leo asubuhi, wakati wa mkutano uliohusu uzinduzi wa taasisi hiyo utakaofanyika leo Hoteli ya Hyatt Regence (Kilimanjaro Hoteli). Kutoka kulia ni Mratibu wa Taasisi hiyo, Rose Majuva, Mwenyekiti, Bahati Geuzye na mmoja wa waanzilishi wa taasisi hiyo, Anna Shanalingingigwa.



 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mratibu wa Taasisi hiyo, Rose Majuva (kulia), akizungumza katika mkutano huo. Katikati ni  Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Bahati Geuzye na Mmoja wa waanzilishi wa taasisi hiyo, Anna Shanalingingigwa.

Na Dotto Mwaibale

CHAMA cha Wanawake Wahasibu Tanzanaia (TAWCA), kitazinduliwa rasmi leo katika Hoteli ya Hyatt Regency (Kilimanjaro jijini Dar es Salaam baada ya kupata usajili.

Hata hivyochama hicho  kimetoa changamoto kwa wanafunzi wa kike kujifunza masomo ya hesabu ,ikiwa ni katika kujiandaa kuwa wahasibu wa badae.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa chama hicho, Bahati Geuzye alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuona wahasibu wa kiume ni wengi kuliko wa kike.

Alisema idadi ya wanawake wanaosoma masomo ya hesabu hawazidi 100 kitu ambacho kimewapelekea wao kuanzisha chama kwa ajili ya kuinua watoto wa kike.

"Ukienda kwenye ofisi nyingi zilizopo nchini wahasibu wanaume ni wengi kuliko wanawake ,ifikie wakati tukiongelea haki sawa basi na sisi tuonyeshe kweli hari ya kutaka kuwa kwenye haki sawa,"alisema Geuzye.

Geuzye alisema wazo la kuanza kwa chama hicho ulianzishwa na bodi ya wahasibu wanawake ikiwa ni katika kumuimarisha mwanamke  na kumfanya ajishughulishe na masuala ya kihasibu zaidi.

Mratibu  wa chama hicho Rose Majuva, alisema  kuwa wamekuja kutoa nafasi kwa wanawake kupewa nafasi za ngazi ya juu ambazo kwa sasa hawazipati.

Majuva alisema watakuwa wakitoa mafunzo mepesi ikiwa ni njia ya kuwafanya wanawake kuelewa na kufanya mambo mazuri .

Alifafanua kuwa wanatarajia kujenga mazinjgira   rafiki kwa ajili ya kusaidia wananwake wahasibu na wakaguzi wa hesabu kufikia malengo yao kitaaluma, kibinafsi na kiuchumi.

"Wanachama watakuwa ni wanawake wenye vyeti vya uhasibu vinavyotolewa na    Bodi  kwa ngazi zote,"alisema Majuva.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)