Pages

Sad News: Mh. Deo Filikunjombe apoteza maisha katika Ajali ya Helicopter Iliyoanguka jana.

Taarifa kutoka kwenye ukurasa wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ukonga na Mjumbe wa NEC CCM, Jerry Silaa unasema kuwa Watu waliokuwa wanatumia helicopter iliyoanguka katika Msitu wa Seluo Jana wamefariki dunia . Katika Helicopter hiyo ambayo ilikuwa ikiendeshwa na Captain William Silaa ambae ni baba mzazi wa Mh Jerry Silaa na Mgombea ubunge wa Jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe nao wamepoteza maisha katika ajali hiyo.

Lukaza Blog inapenda kutoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki kwa kuondokewa na Wapendwa wao

Mungu azilaze roho za marehemu mahala pema peponi Amen

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)