Pages

NBS - Mfumuko wa bei washuka kwa asilimia 6.1

  Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu wa NBS, Ephraim Kwesigabo.
  Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu wa NBS, Ephraim Kwesigabo (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam leo kuhusu, Fahirisi za bei za Taifa kwa mwezi Septembva, 2015.
 Taarifa ikichuliwa na wanahabari.
 Mwanahabari Hilda kutoka gazeti la Daily News akichukua taarifa hiyo kwa umakini zaidi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.

Na Dotto Mwaibale

OFISI ya Taifa ya Takwimu (NBS) imesema mfumuko wa bei  umeshuka hadi asilimia 6.1  kwa Septemba kutoka asilimia 6.4 kwa kipindi cha Agost 2015.

Akizungumza Dar es Salaam leo  Mkurugezi wa Takwimu za Jamii na Sensa ya Watu wa NBS, Ephraim Kwesigabo alisema kushuka kwa mfumuko wa bei kunachangiwa na kushuka kwa  bidhaa za vyakula zinazotumiwa majumbani na kwenye migahawa pamoja na vinywaji baridi.

Alisema mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi kwa Septemba 2015 umepungua hadi kufikia asilimia 9.6 kutoka aslimia 10.2 kwa Agost 2015

''Bidhaa za huduma kwa mwaka huu Septemba umepungua ikilinganishwa na kiasi cha bei kilichokuwepo Agost mwaka uliopita ambapo farihisi za bidhaa zimeongezeka hadi 159.4 na kutoka 149.93 Septemba 2014,' alisema.

Kwesigabo alisema mfumuko wa bei kwa kipimo cha mwaka unapima unapima kiwango cha badiliko la kiasi cha bei za bidhaa pamoja na huduma zote zinazotumiwa na kaya binafsi.

''Mfumuko wa bei ambao haujumlishi bei za vyakula na   na nishati  umebakia kuwa asilimia 22 kwa Septemba 2015 kama ilivyokuwa  Agost 2015,''alisema

Alisema thamani ya shilingi inatafsiriwa katika matumizi ya mlaji wa bidhaa mbalimbali ambapo shilingi ya Tanzania imeonekana kununua bidhaa na huduma zilezile katika vipimo tofauti tofauti.

''Uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma imefikia shilingi 62 na senti 88 kwa Septemba 2015 kutoka Septemba 2010,''alisema.

Mkurugezi huyo alisema farisihi za nishati na mafta zimekuwa na mwendendo wa hali ya juu kwa kipindi chote zikilinganishwa na farihisi nyingine.

Alisema mfuko wa bei kwa kipindi cha mwezi mmoja umeongezeka kwa aslimia 0.1 ukiwa umechangiwa na baadhi ya bidhaa zisizo za vyakula  kama vile mkaa,pamoja na huduma za saluni. 

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)