Pages

MWENYEKITI WA MAKAMPUNI YA PROIN PROMOTION ATEMBELEA BANDA LA WIZARA YA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO

 Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana akifafanua jambo kwa Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotion Ltd Bw. Johnson Lukaza (kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kitaifa mkoani Dodoma leo.Kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Katibu Mtendaji wa Bodi ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya kuigiza Tanzania Bibi. Joyce Fissoo(kushoto) akielezea jambo kwa Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotion Ltd Bw. Johnson Lukaza (wa pili kutoka kushoto) alipotembelea banda la Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo katika maonyesho ya Wiki ya Vijana yanayofanyika kitaifa mmkoani Dodoma leo. Kulia ni Msaidizi wa Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Promotion Ltd Bi. Marrystella Louis.
 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari – MAELEZO sehemu ya Habari Bw. Vicent Tiganya (kulia) akitolea maelezo picha mbalimbali za kumbukumbu ya historia ya Tanzania  kwa Mwenyekiti wa Makampuni yan Proin Promotion ltd Bw. Johnson Lukaza leo mjini Dodoma katika maonyesho ya Wiki ya Vijana kitaifa.Nyuma ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filam Tanzania Bibi. Joyce Fissoo.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Sengerema Sylivester akiangalia baadhi ya Filamu zinazosambazwa na Kampuni ya Proin Promotion ltd leo mjini Dodoma.Kutoka kulia ni Katibu wa Bodi ya Filamu Tanzania Bibi. Joyce Fissoo na M.fanyakazi wa Proin Promotion Bw.Lusubilo Mwanguku
Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania Bw. Sengerema Sylivester akisalimiana na mshindi wa Shndano la kuibua vipaji vya waigizaji (TMT) linaloendeshwa chini ya Kampuni ya Proin Promotion, Bw. Denis Laswai leo mjini Dodoma wakati wa maonyesho ya Wiki ya Vijana ambapo Kampuni hiyo imeshirikiana na Bodi ya Filamu katika maonyesho hayo. Picha na: Frank Shija, WHVUM

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)