Pages

MSANII ORGAN TAI AJA KIVINGINE. AACHIA NGOMA MPYA HUKU PIA AKIBADILI JINA LAKE.

Msanii Organ Tai ambae kwa sasa anajulikana kwa jina la January.
Na:George Binagi-GB Pazzo
Inahitaji majibu zaidi japo mwenyewe ameshindwa kutoa majibu hayo kwa hivi sasa, lakini iko hivi; Msanii Organ Tai kutoka Rock City Mwanza ambae ngoma yake ya kwanza iitwayo Haina Noma ilimtambulisha vyema katika Mikoa ya Kanda ya Ziwa ameachana na jina hilo rasmi.

Akizungumza na BMG (Binagi Media Group), Msanii huyo amesema kuwa sababu za kubadili jina lake atazielezea baadae lakini kwa sasa mashabiki zake wanapaswa kufahamu kuwa ameamua kuwa mpya kwa kila kitu baada ya kuachia wimbo mpya aliofanya na producer Loly Pop kutoka Studio za Min Sound.

"Kwa baadae nitaeleza kiundani zaidi sababu za mimi kubadili jina, lakini kwa sasa mashabiki zangu wanapaswa kujua kuwa nimefanya hivyo baada ya kuachia kwaju langu la pili liitwalo Juhudi ambalo nimefanya na producer Loly Pop kutoka Studio za Min Sound". Alisema Msanii huyo na kuongeza;

"Kikubwa tu kwa sasa Mashabiki zangu wanapaswa kujua kuwa jina langu rasmi la muziki ni JANUARY na siyo Organ Tai kama walivyozoea hapo awali". Alifafanua mkali huyo ambae tayari ngoma yake mpya iitwa Juhudi imeanza kushika kasi katika radio mbalimbali Jijini Mwanza ikiwemo Kiss Fm.

BONYEZA PLAY HAPA CHINI KUSIKILIZA JUHUDI
Kujua Msanii January alikotoka bonyeza HAPA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)