Pages

AKINA MAMA WAJASIRIAMALI KUTOKA MWALO WA SOTA RORYA MKOANI MARA WAPAZA SAUTI ZAO.

Akina mama wajasiriamali kutoka Wilayani Rorya ambapo kulia ni bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na bi.Magreth Steven. 


Akinamama wajasiriamali katika Kijiji cha Sota,
Kata ya Tai iliyopo Wilaya ya Rorya Mkoani Mara, wamewaomba wagombea
watakaobahatika kuingia madarakani katika uongozi wa awamu ijayo, kuwakumbuka
kwa kuwawezesha mitaji yenye riba na mashariti nafuu ili kuendeleza shughuli
zao.


Walitoa ombi hilo wakati wakizungumza na Mtandao
wa BMG (Binagi Media Group), uliowatembelea hivi karibuni ili kujionea shughuli
mbalimbali za uzalishaji mali pamoja na utunzaji wa mazingira zinazofanywa na
wananchi katika ukanda wa Ziwa Victoria Wilayani humo.


“Sisi shughuli tunayoitegemea ni hii tu ya kuuza
dagaa. Tunawafuata mwaloni (Mwalo wa Sota) na kuwaleta hapa (Mwamba dagaa) na
kuwauza kwa watu wengine kutoka katika maeneo mbalimbali ikiwemo nje ya Wilaya hii
(Rorya) kwa ajili ya kwenda kutumia. Alisema bi.Winfrida Joseph ambae ni mmoja
wa akina mama wajasiriamali zaidi ya 20 wanafanya shughuli zao za kuuza daa
katika eneo la Mwamba daa na kuongeza;


“Kiukweli sisi hapa tuna changamoto ya ukosefu
wa mitaji ya uhakika. Hivyo sisi ombi letu kwa hawa wagombea iwe diwani, mbunge
au rais, yeyote yule atakaechaguliwa kuwa kiongozi, tunaomba atukumbuke.
Atusaidie mitaji au kutuunganisha na taasisi zinazotoa mitaji yenye riba na
masharti nafuu kwani masharti ya haya mabenki mengine yametushinda jamani”.


Akinamama wengine akiwemo bi.Magreth Steven waliongeza
kuwa wanaomba kuwepo kwa soko la dagaa la uhakika kama ilivyo kwa samaki katika
mwalo huo wa Sota jambo litakalowasaidia kufanya biashara zao vizuri zaidi kwa
kuwa hawana msaada mwingine zaidi ya kujishughulisha na biashara hiyo ambayo
inawawezesha kupata mahitaji yao mhimu ikiwemo chakula pamoja na kuwasomesha
watoto wao.




Wananchi wa Wilaya ya Rorya ambayo asilimia
kubwa imetawaliwa na ukame kwa vipindi virefu vya mwaka, wanategemea zaidi
shughuli za uvuvi ikilinganishwa na shughuli nyingine kama vile kilimo na
uvuvi.
Kushoto ni Mjasiriamali kutoka Wilayani Rorya, bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na Mteja wake b.Luise Binagi
Kushoto ni Mjasiriamali kutoka Wilayani Rorya, bi.Winfrida Joseph akiwa pamoja na Mteja wake b.Luise Binagi

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)