Pages

WATANZANIA WALIOJITOKEZA HARAMBEE YA CSI UBALOZI WA TANZANIA WASHINGTON DC JUMLA YA $2,696 ZAPATIKANA

Ivan Matovu akisherehesha harambee ya Childbirth Survival International iliyofanywa kwa ushirikiano wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani siku ya Jumamosi Septemba 12, 2015 katika chumba cha mkutano cha Nyerere ndani ya jengo la Ubalozi huo na jumla ya $2,696 zilikusanywa siku hiyo kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya wazazi wanaotarajia kujifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Biharamuro. CSI walishawahi toa msaada wa namna hiyo hospitali ya Amana iliyopo Wilaya ya Ilala jijini Dar na nchini Uganda kwa lengo hilo la kuokoa maisha ya wazazi watarajiwa wa kujifungua. Takribani ya wazazi 35 hufa kila siku aidha kwa sababu ya kukosekana vifaa au kwa uzembe na kutokuwepo kwa elimu ya kutosha itakayosaidia kuokoa maisha ya mzazi hao. Na kama ingekua daladala kila siku inatokea ajali na kuua wa 35 nadhani nchi ingacha shughuli zake na kulitazama swala hilo kwa upana zaidi lakini mtizamo wa akina mama hao 35 wanaopoteza maisha kila siku kwa ajili ya kujifungua bado wananchi na serikali haijalichukulia swala hili uzito unaostahili ya kuokoa maisha ya akina mama hao. PICHA NA VIJIMAMBO NA KWANZA PRODUCTION
 Tausi Swedi mmoja ya waanzilishi wa CSI akielezea kazi kubwa inayofanywa na Childbirth Survival International kujaribu kuokoa maisha ya akina mama wanaojifungua.
 Mkurugenzi na mmoja ya waanzilishi wa CSI nchini Tanzania Mama Stella Mpanda akielezea kazi ya Childbith Survival International nchini Tanzania.
Sandra Kiyonga mmoja wa CSI akielezea jambo.


Jessica Mushala akiipongeza CSI kwa kazi kubwa na nzuri ya kuwasaidia akina mama wanaojifungua Duniani kote kwa kutoa elimu ya uzazi na vifaa kwa wazazi na wakunga kujaribu kuokoa maisha ya wazazi wanaojifungua kutokana na uzembe au kutokua na vifaa ikiwemo elimu ya uzazi.


Kikundi cha utamaduni cha ngoma ya asili aina ya mbuutu ya Uganda ikitumbuiza kwenye harambee hiyo.


Wahudhuriaji kwenye harambee hiyo. Kwa picha zaidi bofya HAPA

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)