Pages

PPF, NHIF WAFANYA BONANZA LA PAMOJA KUONYESHA USHIRIKIANO

 Kipa wa timu ya soka ya Wafanyakazi wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, akichupa kuzuia mpira wa penati bila mafanikio wakati timu hiyo ilipomenyana na ile ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wakati
wa bonanza la pamoja la taasisi hizo mbili lililoandaliwa na PPF na kufanyika kwenye viwanja vya Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam leo Septemba 5, 2015. Katika bonanza hilo ambalo mgeni rasmi alikuwa Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu, zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi wa michezo ya kuvuta kamba, kukimbiza kuku, mbio za magunia, soka na mpira wa wavu. (
Volleyball)

NA K-VIS MEDIA
MFUKO wa Pensheni wa PPF, na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, NHIF, wamefanya bonanza la michezo kwenye uwanja wa Chuo Cha Ustawi wa Jamii, Kijitonyama jijini Dar es Salaam, leo Septemba 5, 2015 ili kuonyesha ushirikiano. Akizungumza kwenye bonanza hilo, mgeni rasmi ambaye alikuwa ni Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, amesema, bonanza hilo limewakutanisha pamoja wafanyakazi wa taasisi hizo mbili za umma, ili kuonyesha mshikamano na ushirikiano sio tu katika Nyanja ya kazi bali pia katika Nyanja
ya michezo na burudani. 

Bonanza hilo lilishirikisha michezo ya kuvuta kamba, soka, mpira wa wafu (Volleyball), mbio za magunia, na kufukuza kuku, ambapo washindi walijinyakulia zawadi mbalimbali. (Picha zote na K-VIS MEDIA/Khalfan Said)
 Mazoezi ya viongo kwa wote
 Mkurugenzi wa Uwekezaji, Mfuko wa Pensheni wa PPF, Steven Alfred, (mbele kushoto), akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo, akioungana na wafanyakazi wa PPF na wale wa NHIF kwenye mazoezi ya viungo
 Mgeni rasmi, Mkurugenzi wa Uwekezaji wa PPF, Steven Alfred, hakuwa nyuma kuwaongoza wafanyakazi wenzake kwenye mazoezi ya viungo
 Mbio za kuku
 Mbio za Magunia
 Mpira wa wavu, (Basketball)
 Mpira wa soka, kati ya PPF, na NHIF
 Meneja Masoko wa PPF, Elihuruma Ngowi, akizungumza na waandishi wa habari kuelezea lengo la Bonanza hilo
 Timu ya soka ya PPF
 Hotuba kutoka kwa Afisa wa PPF
Hotuba ya Afisa Masoko na Elimu kwa Umma, wa NHIF, Sabina Komba

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)