Pages

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO YA WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUDUMU YA UMOJA WA AFRIKA (AU)

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) wakati alipokuwa akiwasili kwenye Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli hiyo uliokuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi. Wa tatu (kulia) ni Jaji Mkuu Mstaafu  Agustino Ramadhan.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia.
 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akikabidhiwa zawadi na Rais wa Mahakama Afrika Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa  Kamati ya Kudumu ya  Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu  kuimarisha demokrasi,  utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Agustino Ramadhan, wakisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya kufunguliwa rasmi jana jijini Arusha.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Mahakama Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika baada ya ufunguzi jana jijini Arusha.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal (kulia) na Rais wa Mahakama Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)