Pages

MAENDELEO ENDELEVU 17 YA DUNIA YAZINDULIWA TANZANIA

IMG_3349
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la UN Women nchini Tanzania, Anna Collins-Falk (katikati) wakipata picha ya kumbukumbu sambamba na mmoja wa wadau wa maendeleo. (Picha na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
UMOJA wa Mataifa kwa kushirikiana na Serikali ya Tanzania wamezindua rasmi malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
Malengo hayo ambayo pia yanajulikana kama malengo ya dunia yamezinduliwa jana Septemba 29 katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Uzinduzi huo ulifanywa na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, na Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame kwa niaba ya serikali, Bi. Fionnuala Gilsenan, Balozi wa Ireland na Bi. Liz Lloyd, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania kwa niaba ya wadau wa mradi wa Project Everyone Partners.
SDGs ni wito wa dunia wa kuchukuliwa kwa hatua za kuufuta umaskini, kuihami dunia dhidi ya uharibifu wa mazingira na kuhakikisha kwamba kila mwanadamu anaishi maisha stahiki katika amani na ustawi.
Katika malengo hayo 17 yapo makusudio 169 yanayotoa ramani ya utengenezaji wa sera za maendeleo na namna ya kutekeleza kwa miaka 15 ijayo.
Malengo hayo yakijengwa juu ya mafanikio ya malengo ya milenia (MDGs), yameingiza vitu vipya kama mapambano dhidi ya tofauti za kiuchumi, ubunifu, mabadiliko ya tabia nchi, lishe, amani na haki. SDGs ni mpango wa dunia unaojikita kwa ustawi wa wanancni na dunia.
IMG_3303
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Awa Dabo (kushoto) na Kiongozi wa mabalozi wa nchi za nje hapa nchini Mheshimiwa Juma Mpango, ambaye ni balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiwa wameshikilia lengo namba 16 na 17 kati ya malengo 17 ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ambayo yamezinduliwa rasmi nchini Tanzania jana 29, Septemba 2015.
Akizungumza umuhimu wa malengo hayo, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez amesema: “Kwa mara ya kwanza katika historia ya dunia , serikali zimekutana na kukubaliana kupeana malengo kwa ajili ya kila mtu. Malengo haya yatasaidia mataifa yote kushirikiana katika kuwezesha ustawi, kupunguza matumizi na kuilinda dunia dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi.Katika hilo watashughulikia elementi zinazohusu maendeleo endelevu: ukuaji wa uchumi, ustawi wa jamii na kulinda mazingira.”
Akizungumzia malengo hayo Bw. Paul Kessy amesema kwamba serikali ya Tanzania ipo tayari kwa malengo hayo.
Alisema kwamba Rais Jakaya Kikwete alikuwa New York, Marekani kwa ajili ya kutia saini malengo hayo na hilo linaonesha ni kiasi gani serikali ya Tanzania iko tayari kushirikiana na wadau wengine kuufuta umaskini.
Pia alisema:“Wakati huu, masuala ya uimarishaji wa muundo wa utekelezaji na kuamsha upya ushirikiano wa kidunia katika maendeleo ni msingi mzuri”
Naye Kamishina wa mipango wa Zanzibar, Bw Ahmed Makame : “Nikiangalia malengo haya 17 ya SDGs, ninafuraha kuona kwamba Zanzibar imekuwa sehemu ya mchakato huu...”.
IMG_3392
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akipozi kwa picha na lengo na tisa kabla ya uzinduzi rasmi wa Malengo ya Dunia kwa Maendeleo Endelevu.
Aidha alisema kwamba Tanzania imeanza vyema katika utekelezaji wa malengo hayo.
Alisema kwa kuangalia uzoefu uliopatikana katika malengo ya milenia, inaonekana namna bora ya kuuoanisha malengo ya kitaifa na ya dunia.
Ninafurahi kusema kwamba Zanzibar tuko katika mchakato wa kutengeneza mkakati wa maendeleo wa kitaifa na tumepanga kufikia malengo ya SDGs.
Akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo, Bi.Fionnuala Gilsenan, amesema taifa lake Ireland lipo tayari kusaidia kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.
“Malengo ya dunia yaliyojengwa katika Malengo ya Milenia yamelenga kukabiliana na matatizo ya zamani kwa mbinu mpya. Zimelenga kukabiliana na tatizo la umaskini na ukosefu wa usawa katika masuala ya uchumi. SDGs haiwezi kufanikiwa bila kuyaangalia masuala ya mabadiliko ya tabia nchi, usawa wa jinsia, haki za biandamu na kukabiliana na mfumo inayobagua.”
Akizungumza kwa niaba ya wadau wa Project Everyone, Bi. Liz Lloyd alielezea umuhimu wa sekta binafsi kushirikiana na Umoja wa Mataifa na serikali ya Tanzania katika kusambaza ujumbe wa malengo ya dunia.
IMG_3397
Mwakilishi wa Shirika la Afya Duniani (WHO), nchini Tanzania, Dk.Rufaro Chatora akipozi la lengo namba 3.
“Kama benki huwa tunazungumza na umuhimu wa kuendelea kuwapo. Huu si tu msemo bali ahadi tunayoishi nayo kila siku. Malengo ya Dunia yanatoa nafasi adhimu ya ushirikiano na taasisi kubwa duniani, kutekeleza malengo 17 kwa nia ya kufufua ushirikiano wa dunia kwa maendeleo endelevu.
Standard Chartered inajisikia furaha ya kuwa nchini Tanzania kwa miaka mingi na inatumaini kwamba kwa ushirikiano huu kila mtu anayeishi nchini hapa atafaidika na maendeleo endelevu ya kiuchumi na kijamii.”
Malengo ya Maendeleo Endelevu yalizinduliwa Septemba 25 wakati viongozi wa dunia walipokutana pamoja mjini New York. Malengo haya yataanza kutumika Januari 1,2016.
IMG_3226
Mkuu wa ushauri wa ufundi wa Mfuko wa Umoja wa mataifa wa Ukuzaji Mitaji (UNCDF), Peter Malika akipozi na lengo na 17.
IMG_3280
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez katika picha ya pamoja na baadhi ya wageni waalikwa kabla ya uzinduzi rasmi wa malengo hayo nchini Tanzania.
IMG_3390
Mtaalam wa mawasiliano kutoka UNFPA, Sawiche Wamunza (kushoto) sambamba na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama katika picha ya ukumbusho.
IMG_3789
Meza kuu katika halfa ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) nchini Tanzania, kutoka kushoto ni Mtaalamu wa masuala ya uchumi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Dar es salaam, Rogers Dhliwayo, Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan, Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy, Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame pamoja na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd.
IMG_3781
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez, akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3554
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered Tanzania, Bi. Liz Lloyd akielezea ushiriki wa benki yake katika utekelezaji wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3580
Kamishina wa mipango (POPC) Bw. Paul Kessy akizungumza kwa niaba ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye hafla ya uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3640
Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame akiwakilisha serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
IMG_3772
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kufanikisha maendeleo.
IMG_3754
Baadhi ya wadau wa maendeleo kutoka mashirika na balozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs) iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
IMG_3796
Baadhi ya wageni waalikwa na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania wakifuatilia maoni na maswali yaliyokuwa yakiwasilishwa kwenye hafla hiyo.
IMG_3829
Mmoja wa wawakilishi wa vijana akiuliza swali meza kuu.
IMG_3868
Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi Duniani (UNHCR), Joyce Mends-Cole akijibu moja ya swali lililoulizwa na kijana (hayupo pichani).
IMG_3857
Sehemu ya wadau wa Maendeleo, taasisi mbalimbali, asasi za kiraia, waandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo.
IMG_3851
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem akifafanua jambo katika kipindi cha maswali na majibu.
IMG_3900
Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi Mkazi wa UNDP Bw. Alvaro Rodriguez (kulia), Kamishina wa Mipango wa Zanzibar, Bw. Ahmed Makame ( wa pili kulia), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Mh. Fionnuala Gilsenan (kushoto) Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Simba Yahaya (wa pili kushoto) kwa pamoja wakifunua pazia maaluma kuashiria uzinduzi rasmi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3912
Sasa yamezinduliwa rasmi.
IMG_3921
Shamra shamra za uzinduzi zikiendelea.
IMG_3950
Fataki zikisherehesha uzinduzi wa malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3975
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko na wadau mbalimbali wa maendeleo, waandishi wa habari wakiwa kwenye picha ya pamoja na vibao vya malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_3997
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Uhuru mchangayiko walioshiriki kutengeneza tangazo maalum la kuelimisha jamii kuhusiana na malengo ya Maendeleo Endelevu 17 ( SDGs).
IMG_4021
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
IMG_4029
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari akiwemo Mwanahabari mkongwe Mama Eda Sanga walioshiriki kwenye uzinduzi huo.
IMG_4097
Bendera ya Umoja wa Mataifa, SDG's na bendera za nchi mbalimbali zikipepea kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
IMG_4078

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)