Pages

Insignia kusaidia jamii katika elimu

Kitendo cha kampuni au taasisi kuisaidia jamii kinageuka kuwa cha kisheria katika baadhi ya nchi na kwa nchi mbalimbali bado ni jambo la uamuzi. 

Watafiti wamegundua, kampuni tatu kati ya kila kampuni nne tayari wanaisaidia jamii au wana mpango wa kuisaidia jamii, miaka michache ijayo. Asilimia 58 ya makampuni yamethibitika kuwa na bajeti kila mwaka kwaajili ya uendelezaji wa shughuli hizi.

Tafiti pia zimeonesha kuwa kwa kiasi kikubwa; Zaidi ya asilimia 80 ya kampuni zina chagua elimu kama eneo muhimu la shughuli zao endelevu.

Kampuni inayoongoza Tanzania kwa uzalishaji wa rangi ya Insignia Limited, inachukulia uwajibikaji kwa jamii kama sehemu muhimu ya sera ya kampuni hiyo. Insignia inatoa mchango mkubwa katika kusaidia jamii ya kitanzania kupitia kujitolea kwake katika elimu.

Kwa mujibu wa Bw. Kishan Dhebar, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Insignia Limited, moja kati ya viashiria muhimu vya maendeleo katika jamii ni elimu. Ambapo pia inachangia jamii kuweza kujitegemea na maendeleo yenye usawa. Pamoja na kuongezeka kwa uelewa wa Dunia juu ya namna gani biashara inachangia katika malengo ya jamii, Insignia Limited imetambua kuwa elimu inahitaji mchango mkubwa zaidi kutoka kwa makampuni.

“Tunaamini kabisa kwamba tunaweza kuleta mabadiliko kwa kutoa misaada kwa wahitaji na wasiojiweza na ndio maana tunatoa msaada sana katika Elimu. 

AnasemaBw. Kishan Mpaka hivi sasa Insignia Limited tumeisadia jamii katika kuendeleza elimu, ikiwa ni pamoja na; kutoa msaada wa kifedha kwa shule ya vipofu na viziwi Ilala, Kutoa kozi chuo cha VETA na vyuo vingine vya ufundi jijini Dar esSalaam, juu ya misingi ya mbinu mbalimbali za upakaji rangi zinazohitajika kitaalamu, na pia kutoa misaada ya kifedha inayohitajika zaidi kwa shule za umma mikoa kama vile Moshi, Dodoma na Dar es Salaam. AnathibitishaBw. Dhebar.

Ingawa inafahamika kuwa utoaji wa elimu ni wajibu wa serikali, makampuni na viwanda vinatoa maendeleo endelevu  ya taaluma, mafunzo na misaada mbalimbali katika sekta  yaelimu.

Mara nyingi, makampuni na jamii kwa ujumla wamekuwa wakikabiliana na changamoto, kama vile ujuzi usioendana na mahitaji, ambapo wanaohitaji ajira hawana ujuzi fulani. Kuondoa changamoto hii Insignia Limited pia imewekeza katika mipango ya mafunzo ambayo yanaimarisha ujuzi wa wa paka rangi wa hapa nchini Tanzania. Kampuni hiyo imezingatia kiwango cha ushindani miongoni mwa mafundi rangi na tangu mwaka 2003 ili kuongeza ufahamu wa kazi yao kwa kiwango kipya. Zaidi ya wapaka rangi 100,000 Tanzania wamepata fursa  ya mafunzo pasipo gharama yoyote kutoka Insignia Limited.

Wapaka rangi walipata maarifa na ujuzi wa hali ya juu kuhusu rangi kama vile rangi ni nini, faida, viungo, kuchanganya rangi, aina mbalimbali za kuta sifa zao na mbinu za upakaji. Mafunzo pia yamekuwa jukwaa la kushughulikia malalamiko kuanzishwa kwa bidhaa mpya, mbinu na hatua za usalama.

Mafunzo haya pia yana thamani kifedha kwa wapakarangi ambapo wanafundishwa mbinu za kuwawezesha kuwa na ufahamu zaidi wa njia bora za kudhibiti gharama ikiwa ni pamoja na kupunguza makosa wakati wa kazi kwaajili ya kufikia matokeo.

Utoaji wa vyeti vya ushiriki mwishoni mwa mafunzo kutoka kwa kampuni inayotambuliwa kumewanufaisha watu wengi zaidi katika kupata ajira.
Mr Kishanan asisitiza kuwa wanaona fahari sana kwa juhudi zao katika shughuli za kujitolea kuisaidia jamii kama kampuni inayoongoza Tanzania kwa uzalishaji wa rangi.

 Pia alieleza juu ya mkakati wao endelevu juu ya uhifadhi na utunzaji wa mazingira. Tunajitoa kwa upande wa elimu na mazingira kitu ambacho binafsi tunakiona kama jambo jema kwa maaendeleo ya biashara kwa ujumla. AnasemaMkurugenzi.

Uwajibikaji kwa jamii unaleta fursa kwa makampuni na serikali. Kupitia kujtolea kwa jamii kampuni na taasisi mbalimbali hutoa mchango wenye manufaa kwa biashara na jamii kwa ujumla.

Kuhusu Insignia Mwaka 1989, Tanzania ilishuhudia kuzaliwa Coral Paints, kampuni ndogo ambayo ingeweza kubadilisha uso wake taya rangi nchini. Ikiendeshwa na dhamira ya kipekee na ubora, kampuni ambayo kwa sasa inajulikana kama Insignia Limited, ilikua kwa kiwango kikubwa na kuvuka mipaka.

Hivileo, Insignia imefikia moja ya malengo yake; ni moja ya kampuni kubwa nchini Tanzania inayoongoza katika utengenezaji wa rangi mbalimbali. Uamuzi wake wakuleta bidhaa zenye viwango vya hali ya juu nchini Tanzania umewezeshwa na ushirikiano na makampuni makubwa ya kimataifa kama Marmoran (Pty) Ltd, iliyopo Africa ya kusini, Ronsea liliyopo nchini Uingereza na Pat’s Deco ya Ufaransa.

Bidhaa mbili za Coral na Galaxy, zinafafanua ubora wa kampuni ya Insignia. Chini ya majina haya, kampuni inatengeneza rangi na bidhaa nyingine nyingi.

Teknolojia ya hali ya juu ipatikanayo katika kampuni hiyo inaipatia kampuni hiyo msaada mkubwa sana katika ushindani. Rangi ya Galaxy inatngenezwa kiufundi,inatumia ujuzi, pembejeo na washauri wa kimataifa, inawapatia wateja wake teknolojia ya kisasa kwenye rangi. Rangi ya Coral paint  ni bidhaa inayoongoza katika soko nchini Tanzania. Imepata kibali, na kuimarisha sifa yake kama bidhaa yenye ubora inayoendana na thamani- ya-fedha.

Kiufanisi, miundombinu ya Insignia inajulikana kwa ubora wake.  Viwanda vyake vina vifaa vyenye ubora na vya kisasa vinavyotengeneza bidhaa zenye viwango vya kimataifa.

Kampuni hii ina viwanda jijini Dar es Salaam, Moshi, Mwanza na Zambia pia ina Vituo vya usambazaji mkoani Moshi, Arusha, Mbeya na Mwanza mikoa mikubwa nchini. Pia kuna uwepo wa mtandao mpana wa wafanyabiashara na malori ya kisasa kuwahakikishia usambazaji wa bidhaa nchini kote. Kampuni hiyo pia ina vituo nchini Rwanda, Burundi na Malawi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)