Pages

UN YAPANDA MITI ZAIDI 2000 KUNUSURU MLIMA KILIMANJARO

Sikiliza kionjo cha hotuba ya Kiswahili ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez hapa chini.


IMG_3361
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge (wa pili kushoto) akiwasili kwenye kijiji cha Marua kata Kiruavunjo, mkoani Kilimanjaro kwa ajili kupanda miti ikiwa ni sehemu ya shamrashamra ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kupokelewa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kulia) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto).(Pichazote na Zainul Mzige wa modewjiblog).
*Sehemu ya Shamra shamra za maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa
Na Mwandishi wetu, Moshi
MASHIRIKA ya Umoja wa Mataifa yaliyopo nchini yameadhimisha miaka 70 ya kuundwa kwa umoja huo kwa kupanda zaidi ya 2000 katika miteremko ya mlima Kilimanjaro.
Kazi ya kupanda miti ilifanywa na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wadau wao ikiwemo serikali ya Tanzania pamoja na wanakijiji.
Kazi ya kupanda miti iliongozwa na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akishirikiana na Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa Nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge.
Shughuli hizo za kupanda miti zilifanyika katika kijiji cha Maruwa.
Akizungumza wakati wa shughuli hiyo Waziri Mahenge alisema kwamba amefurahishwa na hatua iliyochukuliwa na Umoja wa Mataifa ya kuadhimisha miaka 70 kwa kuwakumbusha washirika wao wa maendeleo suala la mazingira.
“Ni kawaida kuadhimisha kuundwa kwa Umoja wa Mataifa Oktoba 24 kila mwaka. Mwaka huu ni tofauti na zaidi ya tofauti umekuwa maalumu kwa namna yake kwa kuwa tunaadhimisha miaka 70 ya uwapo wa Umoja wa Mataifa.” alisema Waziri Mahenge.
IMG_3547
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan akiwasili kwenye sherehe ya kupanda miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa na kusalimiana na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
Hata hivyo alikumbusha kwamba wakati tunaadhimisha miaka 70 ni vyema wadau wa maendeleo wakaangalia historia na kujipanga kimkakati katika kusonga mbele kimaendeleo kwa kujali mazingira.
Alisema kwamba pamoja na hoja ya kujali mazingira pia serikali itaendelea kushirikiana na mashirika ya Umoja wa Mataifa katika mambo mbalimbali ya maendeleo.
Akizungumzia umuhimu wa siku hiyo ya kupanda miti, Rodriguez, alisema kauli mbiu ya wa mwaka huu ni “Sayari Moja Watu Bilioni 7: Utunzaji Mazingira ni Wajibu Wetu”, umerandana na shughuli hizo za upandaji miti.
Alisema kitendo cha upandaji miti kunaonesha wajibu wa kwanza wa kuhami mazingira ya sayari yetu kwa manufaa ya kizazi kijacho cha wanadamu.
Alisema mabadiliko ya tabia nchi si utani yapo kweli na ipo haja ya kuendelea kuwapo kwa juhudi za makusudi za wakazi wa dunia hii kulinda mazingira kwa ajili ya amani maendeleo na ustawi.
IMG_3704
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akisoma hotuba kwa niaba ya Makamu wa Rais kwenye sherehe za upandaji miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
Kwa upande wake balozi wa Ulaya alisema upandaji miti katika mteremko wa mlima Kilimanjaro kuadhimisha miaka 70 ya Umoja wa Mataifa ni alama muhimu katika mapambano ya wanadamu kulinda mazingira.
Alisema ishara hiyo muhimu inaelekeza Umoja huo na wadau wake wa maendeleo kuchukua tahadhari za kutosha kulinda mazingira na inakwenda sanjari na malengo endelevu ya milennia (SDGs) ambayo yana mada tano za kuangaliwa katika mazingira kuliko yale ya awali ambayo yalikuwa na mada moja tu.
Msemaji wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Hoyce Temu alisema kwamba upandaji miti uliofanyika ni moja ya shughuli kadhaa zitakazofanywa na Umoja huo kuadhimisha miaka 70 toka kuanzishwa kwake.
Shughuli nyingine itakayofanywa ni kusafisha soko la Temeke, mashindano ya uchoraji kwa vijana na maadhimisho ya siku yenyewe.
IMG_3676
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe ya upandaji miti kwenye kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.
IMG_3583
Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Balozi Filiberto Sebregondi akizungumza kwenye sherehe ya upandaji miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa zilizofanyika mkoani Kilimanjaro.
IMG_3386
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy na Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya wakifuatilia hotuba mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye sherehe hizo.
IMG_3403
Wakufunzi kutoka chuo cha Ualimu Moshi wakitoa burudani kwenye hafla ya kupanda miti katika kijiji cha Marua ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_3381
Pichani juu na chini ni baadhi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na wanakijiji wa kijiji cha Marua walioshiriki sherehe za upandaji miti ikiwa ni Shamra shamra ya kusheherekea miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_3384
IMG_3748
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akipanda mti katika kijiji cha Marua karibu na miteremko ya mlima Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa yaliyofanyika mkoani Kilimanjaro.
IMG_3774
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akipanda mti katika kijiji cha Marua mkoani Kilimanjaro, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 70 ya Umoja wa Mataifa, kila mti unaashiria kila mwaka ambapo Umoja wa Mataifa umekuwa ukileta maendeleo duniani ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi. Kushoto ni Mshehereshaji Afisa Misitu wa mkoa wa Kilimanjaro, Emanuel Kiyengi.
IMG_3825
Afisa Misitu wa mkoa wa Kilimanjaro, Emanuel Kiyengi (kulia) akitoa maelezo kwa mgeni rasmi, mabalozi na viongozi wa serikali katika eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kupanda miti 200 zoezi lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa nchini katika kusheherekea miaka 70 ya Umoja wa Mataifa.
IMG_3829
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akiteta jambo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
IMG_3781
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge (wa tatu kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa eneo maalum lililotengwa kwa ajili ya kupanda miti 2000 katika kijiji cha Marua karibu na miteremko ya mlima Kilimanjaro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (wa pili kushoto), Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kushoto), Mkuu wa mabalozi, ambaye pia ni Balozi wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Juma Halfan Mpango (wa nne kushoto), Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan (wa tano kushoto), Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya, Balozi Filiberto Sebregondi (wa nne kulia), Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga ( wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy ( wa pili kulia) pamoja na Afisa Tawala Mkuu katika ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Omari Msuya.
IMG_3795
Mkuu wa wilaya ya Moshi, Novatus Makunga akishiriki zoezi la kupanda miti katika kijiji cha Marua.
IMG_3294
Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kushoto) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues (kulia) wakati wa zoezi la upandaji miti.
IMG_3290
Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akishindilia udongo kwenye mti aliopanda katika eneo lake.
IMG_3346
Kaimu Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo (UNDP), Titus Osundina akishiriki zoezi la upandaji miti katika kijiji cha Marua mkoani Kilimanjaro.
IMG_3803
Balozi wa Ireland nchini Tanzania, Bi Fionnuala Gilsenan akishiriki zoezi la kupanda miti lililoendeshwa na Umoja wa Mataifa ikiwa ni sehemu ya kusheherekea miaka 70 tangu kuanzishwa kwake duniani.
IMG_3810
Afisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akishiriki zoezi la kupanda mti katika kijiji cha Marua.
IMG_3844
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem na Beatrice Mkiramweni kutoka ofisi za Mratibu Mkazi wa UN Tanzania wakipanda picha ya kumbukumbu kwenye mti walioshirikiana kupanda.
IMG_3864
Wakinamama wa kijiji cha Marua wakipozi miti yao wakati wakielekea kuunga mkono juhudu za Umoja wa Mataifa katika kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi.
IMG_3275
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem.
IMG_3342


Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (kulia) wakitazama jambo na Mkuu wa ofisi ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues wakati wa zoezi la kupanda miti katika miteremko ya mlima Kilimanjaro kijiji cha Marua mkoani Kilimanjaro.
IMG_3577
Baadhi ya maafisa wa Wizara ya Mambo ya Nje na Umoja wa Mataifa wakijadiliana jambo na mshehereshaji wa hafla hiyo.
IMG_3883
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akikata utepe kuzindua jiwe la kumbukumbu la miaka 70 ya Umoja wa Mataifa kwenye eneo maalum lililopandwa miti 2000 katika kijiji cha Marua, mkoani Kilimanjaro. Wanaoshuhudia tukio hilo ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia), mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali.
IMG_3886
Zoezi la uzinduzi likiendelea.
IMG_3888
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la kumbukumbu la miaka 70 ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania.
IMG_3898
Mgeni rasmi Mwakilishi wa Makamu wa Rais, Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Mazingira, Binilith Mahenge katika picha ya pamoja na mabalozi waalikwa, viongozi wa Serikali na wakuu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa Tanzania.
IMG_3904
Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na mgeni rasmi.
IMG_3847
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani (UNFPA) nchini, Dkt. Natalia Kanem akipata picha ya kumbukumbu na wanakijiji wa kijiji cha Marua.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)