Pages

Uchaguzi Ubunge Jimbo la Handeni lawaka moto


“Kimsingi hakuna mgombea anayejua amepata kura ngapi na wapi amekosa, maana hata huyo Salu anayedaiwa ameshinda amepewa ushindi wa jumla na hakuna anayejua namna  gani mchakato huo umefanyika, ndio maana ofisi ya CCM wilaya iliamua kufanya  siri, huku kila mgombea akiambiwa jambo la kumpa moyo,” alisema Mbwana.

Naye Chifu Msopa alisema kwamba hawawezi kukubali mtu mmoja afanye mambo kwa maslahi yake, hivyo wagombea wote wa ubunge watasusia mchakato wa kampeni katika jimbo la Handeni, kama hali ya kubebana itaendelea dhidi ya Katibu na washindi wake aonao wanafaa kuliko wengine.

“Hatutaki kuendelea kuwa waoga huku wachache wakiendelea kuiharibu CCM yetu, uchaguzi huu urudiwe au kufuata maagizo ya Kamati ya Siasa ya wilaya na ile ya Maadili ambayo kwa bila kujua kwanini, Katibu aliyaweka kando mapendekezo hayo na kufanya anavyotaka mwenyewe,” alisema Msopa.

Kwa kipindi cha wiki moja sasa jimbo la Handeni limekuwa kwenye mgogoro mkubwa kati ya viongozi wa CCM wilaya ya Handeni na wagombea ubunge ambao kwa kiasi kikubwa wameonyesha kuchukizwa na mwenendo mbovu wa katibu wa CCM handeni, ambaye ameendelea kuwabeba wagombea, wakiwamo wale waliotajwa kwenye kashfa za rushwa.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)