Pages

TPB YAZINDUA RASMI KADI YA ATM KWA KIKUNDI CHA VICOBA ENDELEVU

 Rais wa VICOBA Endelevu, Devota Likokola, (Watatu kushoto), akinyanyua juu, mfano wa ATM kadi ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, wakati wa uzinduzi wa kadi hiyo itakayotumiwa na wanachama wa VICOBA Endelevu kota nchini. Uzinduzi huo ulifanyika leo Agosti 15, 2015 kwenye bustani
ya kumbukumbu ya mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, Mwenyekiti wa Bodi wa Wadhamini ya Benki hiyo, Profesa Lettic Rutashobya, na Katimu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezweshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, Beng’ Issa.(Picha na Habari na K-VIS MEDIA)

BENKI ya Posta Tanzania, TPB, imezindua rasmi kadi maalum ya ATM kwa ajili ya wanachama wa kikundi cha, VICOBA Endelevu.
Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika kwenye bustani ya kumbukumbu ya Mashujaa, Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, Agosti 15, 2015, ambapo Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TPB, Profesa Lettic Rutashobya, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi, pamoja na Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, (NEEC), Beng’ Issa, walishuhudia Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, akimkabidhi mfano wa kadi hiyo ya ATM, Rais wa Vicoba Endelevu, Devota Likokola mbele ya mamia ya wanachama wa Vicoba Endelevu kutoka sehemu mbalimbali nchini.

Benki ya Posta Tanzania, imeingia mkataba na Vicoba Endelevu, wa kuwapatia mikopo midogomidogo wananchama hao chini ya udhamini wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi, NEEC, ili kukuza mitaji na kuendeleza shughuli zao za kiuchumi.
 Wana VICOBA Endelevu wakiingia kwenye bustani hiyo kwa maandamano
 MWENYEKITI wa Bodi hya Wadhamini ya Benki ya Posta Tanzania, TPB, Profesa Lettic Rautashobya, (katikati), Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TPB, Moses Manyanta, na Meneja Mkuu wa TPB anayeshughulikia masuala ya kampuni, Noves A. Moses
 Profesa Lettic, na Katibu Mtendaji wa NEEC, Beng' Issa, wakitembelea shughuli za wajasiriamali ambao ni wanachama wa VICOBA Endelevu
 Profesa Rutashobya, akizungumza na waandishi wa habari
 Beng' akizungumza na waandishi wa habari
WAELIMISHAJI kuhusu shughuli za ujasiriamali wa VIDOBA Endelevu, wakipozi kwa picha

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)