Pages

SIMBA SPORT CLUB YAWA ZAWADIA MASHABIKI WAKE

Rais wa Simba Sport Club Evans Aveva  wa tatu kutoka kushoto akiwa na Washindi wa bahati nasibu  Pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Eaggroup ImanKajula kushoto na Msemaji wa Timu hiyo Manara
Rais wa Simba Evans Aveva Akikabidhi Zawadi kwa Mmoja wa Washindi
Uongozi wa klabu ya Simba leo umetoa zawadi kwa washindi wa bahati na sibu iliyochezeshwa siku ya Simba Day Aosti 8 mwaka huu wakati wa kilele cha sherehe za siku ya Simba Day zilizofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Zawadi zilizo kabidhiwa kwa washindi ni jezi pamoja simu, kila mshindi amepata jezi ya juu pea moja pamoja na simu moja aina ya Motec. Washindi wa zawadi hizo ni Jeremia Venist, Ahazi Mwembe pamoja na Marko Mgimba.
Washindi wa bahati nasibu  wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao
Mbali na zawadi hizo, klabu hiyo pia imekabidhi mipira nane kwa shule mbili za msingi za mkoa wa Dar es Salaam ambapo Shule ya Msingi Mikocheni A imepata mipira minne huku Shule ya Mingi Chang’ombe Mazoezi nayo ikikabidhiwa mipira minne.
Rais wa Simba Evans Aveva akimkabidhi mpira mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mikocheni A
Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema, klabu hiyo inataka kusaidia soka la vijana nchini na kwasasa wameanza na mkoa wa Dar es Salaam lakini baadae watasonga mbele hadi kwenye mikoa mingine ili kuwafikia watu wengi zaidi hasa watoto ambapo ndio leno hasa la klabu hiyo kusaidia soka la vijana.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)