Pages

Simba day yafana huku Simba wakikubali kichapo Kutoka Kwa SC Villa Ya Uganda taifa


 RAIS wa klabu ya soka ya Simba, Evans Aveva, (pichani juu), jana alikuwa kama kocha wa Chelsea, Josse Morinho, kutokana na jinsi alivyokuwa akiwaelekeza wachezaji wa timu ya viongozi wa Simba dhidi ya timu ya soma ya wasanii wa bongo movie na bongo flava kwenye maadhimisho ya siku ya Simba almaarufu kama Simba Day.


Aveva ambaye alikuwa “kaulamba” yaani kapiga suti yake nyeusi, alikuwa ndio “kocha wa timu hiyo ya viongozi wa Simba. Akiwa amevalia suti nyeusi, hakuweza kutulia kwenye kiti, kila wakati alisimama na kuwaelekeza wachezaji wake kwa kunyoosha mikono na kufoka. Timu ya soka ya viongozi wa Simba iliibuka mshindi wa bao 1-0.

Baada ya pambano hilo, lilifuatia tendo la kuwatambulisha wachezaji wapya wa Simba na benchi la ufundi kabla ya kuanza kwa pambano maalum la kirafiki baina ya timu hiyo ya mtaa wa Msimbazi jijini Dar es Salaam na wageni wao Sports Club Villa ya Uganda, katika pambano hilo la kirafikli, Simba iliibanjua Sports Club Villa "Jogoo" bao 1-0. Bao lililofungwa na Awadh Juma, kwenye dakika ya 45 ya kipindi cha lala salama.
 Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Hassan Dalali(kulia)
 Kikosi cha timu ya wasanii
 Kikosi cha timu ya viongozi wa Simba
 Aveva katika "ubora" wake
 Ben Kinyaiya, (kulia) wa timu ya wasanii, akiumiliki mpira mbele ya Imani Kajula
 JB akiwatoka wachezaji wa timu ya viongozi wa Simba
 JB akifuatilia jinsi wenzake wanavyopelekwa puta na timu ya viongozi wa Simba
 Kocha mkuu wa Simba, katika "ubora" wake
Kocha Mkuu wa Simba, akizungumza jambo na mchezaji wake, Hamisi Kiiza Diego
 Mgeni rasmi, wa Simba Day, Mohammed Dewji "MOD", akisalimiana na mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi
 Mo akisalimiana na wachezaji wa timu ya Sports Club Villa ya Uganda
 Kikosi cha timu ya Sports Club Villa, kilichomenyana na Simba na kuangukia "pua" kwa kunyukwa bao 1-0
 Kikosi kipya cha Simba, kilichoinyuka Sports Club Villa
Mashabiki wa Simba wakiishangilia timu yao
Aveva katika "ubora" wake
Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara, ni mmoja wa watu "waliovunjwa mbavu" na Aveva
Msemaji wa Simba, Haji Sunday Manara, (kushoto), akionyesha "kumbe wamo"
Imani Kajula, (kulia), wa timu ya viongozi wa Simba, akijaribu kuutuliza mpira
Mchezaji wa kiungo wa timu ya Wasanii JB, akiusaka mpira katikati ya uwanja
Ibrahim Masoud, "Maestro" akipiga hesabu wakati wa pambano kati ya timu ya soka ya viongozi wa Simba na ile ya wasanii
Mshambuliaji wa Simba, Khamisi Kiiza "Diego", (kulia), akijaribu kuupiga mpira huku akichungwa na msitu wa walinzi wa SSC Villa kutoka Uganda

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)