Pages

Mtego wa Panya ulipowanasa mbuzi, jogoo na Ng'ombe


Kuna mtego wa panya uliosababisha madhara hata kwa wasio panya. Panya kwenye nyumba aliubaini mtego wa panya uliowekwa na mwenye nyumba uvunguni mwa kitanda. Panya yule akamwendea jogoo wa mwenye nyumba. Akamwambia: “Ewe jogoo, kuna mtego umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane namna ya kuutegua kabla haujatudhuru wote."

Jogoo akajibu
"Ondoka zako, mie mtego wa panya unanihusu nini wakati sina kawaida ya kufika uvunguni mwa kitanda?"


Panya yule akaenda hadi kwa mbuzi wa mwenye nyumba. Akamwambia: "Ewe mbuzi mwema, unajua kuna mtego wa panya uvunguni mwa kitanda cha mwenye nyumba. Tusaidiane mawazo ya kuutegua kabla haujatudhuru sote."


Mbuzi akajibu
"Hivi tangu lini ukaniona nikiingia chumbani kwa mwenye nyumba? Mtego huo wa panya haunihusu mie mbuzi." Panya akaenda hadi kwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Akamwambia: "Ewe ng'ombe wa Bwana, kuna mtego wa panya umewekwa uvunguni mwa kitanda. Tusaidiane mawazo namna ya kuutegua kabla haujatuletea madhara."


Ng'ombe akajibu akionyesha mshangao; "Sijapata kusikia jambo la ajabu kama hilo. Yaani, mie ng'ombe nidhurike na mtego wa panya ulio uvunguni mwa kitanda! Hilo halinihusu."
Basi, ikatokea siku moja, nyoka akaingia chumbani kwa mwenye nyumba. Katika kutambaa kwake uvunguni mwa kitanda, mkia wa nyoka ukanasa mtegoni. Kishindo kilisikika. Mwenye nyumba alikwenda kwa furaha akiamini hatimaye panya aliyekuwa akimsumbua sasa amenaswa. Hapana, ni nyoka aliyenaswa mkia. Na ni mwenye hasira pia. Akamng'ata mguu. Sumu kali akamwachia. Mwenye nyumba akafa.


Jirani wakafika msibani. Siku ya kwanza watu walikuwa wachache. Wakahitaji kitoweo. Akakamatwa jogoo wa mwenye nyumba. Jogoo akachinjwa. Siku ya pili watu wakaongezeka. Kilihitajika kitoweo pia. Akakamatwa mbuzi wa mwenye nyumba. Mbuzi akachinjwa. Na siku ya maziko watu wakawa wengi zaidi. Akakamatwa ng'ombe wa mwenye nyumba. Naye akachinjwa!


Ni jogoo, mbuzi na ng'ombe wa mwenye nyumba walioamini kuwa madhara ya mtego ule wa panya yasingewahusu wao. Walikosea. Panya alikuwa sahihi, na walamtego haukumdhuru panya!
Kuna cha kujifunza kutoka kwenye kisa hiki. Wale watz ambao akishajenga kanyumba kake akaweka na fens bas anajidai siasa hazimuusu bas anakua kama hawo jogoo, mbuz na ng'ombe.

Mambo mengi unayodhani hayakuhusu kuna siku uatakuhusu pasipo kujua yamekuhusuhusu vipi.

No comments:

Post a Comment

Tafadhari Maoni Yenye Matusi Hayatakuwa Publish Tutoe Maoni Bila Kuumiza Wala Kujeruhi Hisia Za Mtu.....@(Sponsored By Lukaza Blog)